Mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka((CCM)katikati akizungumza katika hafla ya kukabidhi pikipiki 14 kwa Naibu Katibu Mkuu Taifa Rodrick Mpogolo kwa ajili ya makatibu Kata 14,hafla hiyo ilifanyika juzi Mjini Kibaha .picha na Gustaphu Haule
.............................................................


MBUNGE wa Kibaha Mjini Silvestry Koka (CCM)amekisaidia chama chake kwa kutoa msaada wa pikipiki mpya 14 na gari moja la kubebea wagonjwa ikiwa na jumla ya thamani zaidi ya Sh.milioni 43.mwandishi Gustaphu Haule anaripoti toka Pwani

Koka,alikabidhi msaada huo kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Rodrick Mpogolo ,katika mkutano mkuu wa CCM Kibaha Mjini uliofanyika kwa ajili ya kueleza namna ilani ilivyotekelezwa kwa muda wa miaka minne iliyopita.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo Koka,alisema kuwa lengo la kutoa vitendeakazi hivyo ni kuwasaidia makatibu Kata 14 wa Kibaha Mjini kupata urahisi wa kufanyakazi zao.

Koka alisema makatibu wa Kata ndio watendaji wakuu wa chama na kwamba kwa muda mrefu walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya usafiri hivyo ameona ni vyema awasaidie kupata usafiri.

Alisema kuwa, pikipiki hizo ni mali ya CCM na kwamba hata kama Katibu wa Kata husika atang'atuka madarakani mali hiyo itabaki katika Kata kwakuwa imetolewa kwa ajili ya kuimarisha chama. .

"Makatibu hawa walikuwa wanakabiliana na changamoto ya usafiri na hii ilikuwa inasababisha kazi nyingi za chama kushindwa kufanyika kwa wakati hivyo nikaona ni vyema nikawasaidia kutatua kero hiyo kwa faida ya chama chetu,"alisema Koka.

Aidha Koka alisema kuwa mbali na pikipiki hizo lakini ataendelea kushirikiana na Wananchi,wanachama pamoja na viongozi katika kuhakikisha wanatatua kwa pamoja changamoto zilizopo.

Kwa upande Mpogolo, alimshukuru mbunge huyo kwa hatua ya kusaidia vitendeakazi hivyo huku akiongeza kuwa anaamini pikipiki zitakuwa ni chachu ya ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2020.

Mpogolo, aliwataka makatibu hao kutumia vitendeakazi hivyo kwa kufanyakazi ya chama na sio vinginevyo na kama itagundulika mtu anatumia kinyume na malengo yaliyowekwa ni wazi kuwa watamnyang'anya.

Hatahivyo,mwenyekiti wa CCM Mkoa Pwani Ramadhani Maneno,alisema kuwa Koka ametoa pikipiki hizo kwa ajili ya kukitumikia chama kwa nafasi yake lakini chama kipo tayari kumpokea mtu yeyote mwenye nia njema ya kukisaidia Chama.

Maneno,alisema kuwa kama kuna mwanachama anataka kukisaidia chama anapokelewa lakini lazima afuate njia sahihi na kwa utaratibu maalum na kama kuna mtu anatoa bila kufuata utaratibu huyo lazima achukuliwe hatua.

Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: