Mkuu wa wilaya Ilala Dkt. sophia Mjema akisalimiana na Katibu wa Umoja wa Wanawake Kata ya Tabata Tatu Seleman hivi karibuni

Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus akiangalia biashara za Wanawake kata ya Kiwalani hivi karibuni
.......................................................
Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam Dkt. Sophia Mjema anatajia kuwa mgeni ni rasmi kwenye Kongamano la Umoja wa Wanawake Tanzanua (UWT) Kata ya Tabata litakayofanyika Ijumaa Machi 27 mwaka huu kwenye ukumbi wa Latino Inn.

 kongamano hilo litaongozwa na mkuu wa Wilaya Dkt Mjema na Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus kuanzia saa mbili asubuhi ambapo siku hiyo kutakuwa na maonesho ya wanawake wajasiriamali yatakayotangulia na shughuli za kijamii.


Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu wa Kongamano hilo   Mjumbe wa Halmashauri kuu Tabata Mtambani Heri Shaaban alisema  maandalizi yote yamekamilika kufanikisha siku hiyo  kwa kushirikiana na UWT Tabata.

Heri alisema wengine watakaopamba siku hiyo Warembo wa Miss Ilala   na madiwani Wanawake wa halmashauri ya manispaa ya Ilala.

"Kongamano la kwanza la siku ya Wanawake Tabata limeandaliwa na mimi kwa kutambua mchango wa wanawake na vijana  wilayani Ilala, Octoba 05/2019 nilitununikiwa tuzo na mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete tuzo ya Ubunifu ya maswala ya Wanawake na vijana iliyotolewa na Utalii 255 Tanzania ambapo Mwenyekiti wake Mbunge Angelina Malembeka  tuzo hii ndio  imenipa hamasa kuwaanda jambo hili kwa siku hii muhimu kufurahi na wanawake wa Tabata hususani kata ya Tabata " alisema Heri.

Aidha alisema siku hii muhimu kwa Wanawake wa Tabata kuelezea changamoto zao sambamba pia watapata elimu ya malezi kwa vijana kuhusiana na elimu ya Afya ya  uzazi kutoka kwa wataalamu ofisi ya Mganga Mkuu pamoja na elimu ya ujasiriamali na mikopo kutoka kwa Afisa maendeleo Manisipaa ya Ilala.

Aidha Mratibu Heri Shaaban alisema Kata ya Tabata hilo ni kongamano la kwanza la siku ya Wanawake ambapo litakuwa endelevu kila mwezi March.


Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: