Na Esther Macha, Mbeya
TAASISI isiyokuwa ya kiserikali  ijulikanayo kama elimu kwa vijana  kupitia michezo (YES TZ) imepokea msaada wa Ruzuku  ya Dolla za kimarekani 42,000 sawa  na sh. Mil.97,012,986.775 kwa ajili ya matumizi ya kuijengea taasisi uwezo ili iweze kutekeleza majukumu yake ya kusaidia serikali kufikia malengo yake mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ,Kenneth Simbaya alisema  Ruzuku hiyo imetolewa  kutoka Open Society Initiative for Eastern Africa (OSIEA) na kwamba fedha hizo zitatumika kuanzia January 2020 mpaka June 30,2021.
Alisema kupitia waelimishaji rika wa kujitolea wa taasisi hiyo kumekuwa na ongozeko kubwa la vijana  ambao wamepata mafunzo  toka kwa vijana wenzao wanaojitolea.
Aidha Simbaya alisema waelimishaji rika hao wameweza kupeleka elimu sahihi  kwa vijasna wenzao ambayo imekuwa  msaada mkubwa.
Alisema kuwa vijana 4000 walifikiwa na vijana wa kujitolea na wengi  wao ni wanawake kutoka kata tisa(9).
 Kwa upande wake Mwelimishaji  rika wa kujitolea ,Katie Dunbar alisema kuwa kujitolea kuna faida kubwa  sana kwa vijana  kwani wanajifunza vitu vingi sana na kupata uzoefu wa kufanya kazi.
“Mfani mimi  mwenyewe hapa nimejinza vitu vingi kwa kujitolea ukiachilia mbali kupata  uzoefu wa kujitolea kufanya kazi kumeniwezesha kukuza mtandao wa watu ninao wafahamu ambao ni muhimu katika maisha yaqngu ya kikazi  pamoja na kuongeza marafiki”alisema Dunbar.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: