Friday, 21 February 2020

WAZIRI MKUU ATAKA UMAKINI KATIKA UTOAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA MIKOA YA MIPAKANINa Editha Karlo,Kigoma
WAZIRI Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ameagiza umakini ufanyike katika utoaji wa vitambulisho vya Taifa hususani katika Mikoa iliyopo mipakani ili kuimarisha usalama wa nchi.

Majaliwa ameyasema hayo leo wakati akiongea na wajumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu chama cha mapinduzi(CCM)ya Mkoa wa Kigoma kuwa  kumekuwepo na malalamiko ya wananchi wanaofuatilia vitambulisho vya Taifa wanadaiwa siyo raia wa Tanzania hivyo hupata usumbufu katika kupata vitambulisho hivyo.

"Katibu wa chama na MNEC  ameniambia hapa wananchi waliojitokeza kujiandisha ili kupata vitambulisho vya Taifa kwa Mkoa wa Kigoma ni wachache hasa maeneo ya mipakani ambapo wanapata usumbufu wa kupata vitambulisho hivyo kwasababu ya mashaka ya uraia wao"alisema

Waziri Mkuu ambaye pia ni mlezi wa chama cha mapinduzi(CCM)kwa Mkoa wa Kigoma aliwataka idara ya uhamiaji wafuatilie kwa makini lazima usalama wa nchini usimamiwe ipasavyo hususani katika mikoa ya mipakani na lazima tujiridhishe kuwa anayepata kitambulisho cha Taifa ni mwenzetu"alisema

Alisema kila mtanzania aliyeomba kitambulisho cha Taifa atapata na hata wale ambao line zao za simu zimeshazimwa ambao ni watanzania nao pia watapata na hakuna atakayepoteza haki zake.

"Tumeamua kusajili namba za  simu kwaajili ya usalama,zamani ili kuwa mtu ananunua line ya simu afu anatukana mtu akimaliza anaitupa sasa hivi hakuta kuwa na hicho kitu"alisema

"Watanzania mnatakiwa kuwa makini msiruhusu watu wasio na nia njema  kuingia nchini kwa njia za panya pia mtu ambaye siyo mtanzania kujiandikisha na kupata kitambulisho cha Taifa"alisema

Alisema zoezi hili la kupata vitambulisho lifanyike vizuri na wataharakisha ili wananchi waweze kupata vitambulisho kwani serikali itaongeza watendaji na vifaa katika Wilaya zote ili waweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Pia amewataka viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi(CCM)wahimarishe ushirikiano miongonu mwao na pale kwenye dosari wazirekebishe kwasababu hakuna jambo lisiloweza kutatuliwa.

"Lazima tuhakikishe chama kinabakia salama na kinaendelea kushika dola hivyo ni wajibu wa kila mwanachama kuhakikisha tunafikia malengo hayo"alisema
 MWISHO

No comments:

Post a comment