Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Februari 26,2020 katika ukumbi wa NSSF Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Meneja Mahusiano na Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu  Dk. Zumbi Musiba akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Talaba akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe, Jasinta Mboneko ( wa kwanza kulia) wakiwa ukumbini.
Meza kuu wakifuatilia matukio ukumbini.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Dk. Meshack Kulwa akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Mstaafu Emmanuel Maganga. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa.
Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.

Naibu Waziri wa  Ujenzi Elias Kwandikwa akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.

Naibu Waziri wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mkutano unaendelea.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Stephen Masele akizungumza katika Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki.
Mkutano unaendelea.
Viongozi wa dini wakifuatilia mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkutano unaendelea.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Mhe. Angellah Kairuki ameongoza Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanya biashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuboresha biashara ili kuongeza wigo wa ajira kwa vijana na kulipa kodi kwa hiari. 
Mkutano huo umefanyika leo Jumatano Februari 26,2020 katika Ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na Manaibu Waziri kutoka Wizara Mbalimbali,Wabunge wa mkoa wa Shinyanga,viongozi wa serikali,siasa,taasisi za fedha,wafanyabiashara,wawekezaji na wadau mbalimbali wa maendeleo. 
Akizungumza katika Mkutano huo,Kairuki  aliwataka wafanyabiashara na wawekezaji wanapokuwa na migogoro wasisite kuwasiliana na serikali ili kuitatua na kuepuka kusababisha migogoro kuwa mikubwa. Kairuki alitumia fursa hiyo kuipongeza serikali ya mkoa wa Shinyanga kwa kutenga jumla ya hekta 200 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo na hekta 640 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vikubwa katika eneo la Bukondamoyo kata ya Zongomela wilayani Kahama ambalo tayari serikali imetumia shilingi 809,400,000/= kwa ajili ya kuliwekea miundombinu wezeshi ikiwemo barabara,umeme na maji. "Kuhusu suala la Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli nitalifuatilia kwa ukaribu kwani limelalamikiwa kuwa changamoto kwa wafanyabiashara",alisema Kairuki.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack alisema mkoa wa Shinyanga umefanya jitihada kubwa ya kuvutia Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambapo hadi sasa kuna jumla ya Viwanda 729 kati ya hivyo,Viwanda Vikubwa ni 13,viwanda vya kati 11 na viwanda vidogo 705 ambavyo vimeajiri wafanyakazi 10,150. 
Telack alisema mkoa wa Shinyanga umetenga jumla ya hekta 20,289.25 kwa ajili ya uwekezaji kwenye sekta ya biashara,kilimo na viwanda kati ya hekta hizo, Halmashauri ya Mji wa Kahama imetenga hekta 2,000, Shinyanga 5,560, Ushetu 2,110,Kishapu 10,361.70 na Msalala hekta 257.53. 
Hata hivyo kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaozaliwa na wanaohamia Telack alisema hali hiyo imesababisha uhitaji wa ujenzi wa shule,vituo vya huduma za afya,ujenzi wa nyumba za kulala wageni na kadhalika. 
“Serikali imetengeneza mazingira wezeshi kwa wazawa kuingia kwenye biashara ya Madini ya almasi kwa kuuelekeza Mgodi wa Almasi wa Mwadui (WDL) kuuza asilimia 5 ya almasi inayozalishwa ndani ya soko la ndani kwa njia ya mnada na uuzaji wa kawaida.Natoa rai kwa wafanyabiashara wote kuchangamkia fursa hii ili baadaye almasi yote inayozalishwa iuzwe ndani ya mkoa wetu na kuongeza ukuaji wa wa uchumi wa mkoa”,alisema Telack.
Naye Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema serikali itayafanyia kazi malalamiko ya wafanyabiashara ikiwemo tozo nyingi huku akisisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kulipa kodi.
Kwa Upande wake,Meneja Mahusiano na Maendeleo ya Jamii Mgodi wa Bulyanhulu  Dk. Zumbi Musiba akimwakilisha Mkurugenzi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick, alisema Barrick inashukuru kwa fursa ya kufadhili Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali,Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mkoa wa Shinyanga ili kushirikiana na serikali kuchangia katika kuendeleza uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla.
"Wengi wa washiriki wa mkutano huo ni wadau wa Kampuni ya Barrick hivyo hiyo ni fursa nzuri ya kusikia wanakabiliwa na changamoto zipi ili kwa pamoja tuweze kuzitafutia ufumbuzi",alisema Dk. Musiba.

Mkutano huo umeandaliwa na Kamati Tendaji ya Baraza la Biashara mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na kamati ya maandalizi ngazi ya taifa kwa ufadhili wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya Barrick, Benki ya CRDB,NMB, TPB na NBC. 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: