Monday, 24 February 2020

wazazi watakiwa kuwekeza katika elimu


Na Esther  Macha,Chunya
WAZAZI na walezi katika Mji wa Makongolosi Wilayani Chunya Mkoani mbeya wametakiwa kuendelea kuwekeza katika elimu kwa manufaa ya watoto wao  na kwa maisha ya badae na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa jana  na  Mkurugenzi wa shule ya awali  na msingi kwa  mchepuo wa kingereza ya Holy Land ,Lawena Nsonda (Maarufu kwa jina la Baba Mzazi)wakati  akizungumza  na Msumba News kuhusiana na suala la elimu kwa watoto  na kufurahishwa na mwamko uliopo  hivi sasa kwa wazazi ukilinganisha na miaka ya nyuma ilivyokuwa .
Nsonda alisema kuwa kwa Mji wa Makongolosi wanajivunia hivi sasa wazazi jinsi walivyo sasa suala la elimu wamelipa kipaumbele sana ,hii ni hatua kubwa sana.
“Tunajivunia sana hasa ukizingatia hivi sasa tumefungua hii shule ambayo kwa mji huu ni ya kipekee  tunaamini kwamba italeta mabadiliko makubwa kwa wazazi na walezi wa Mji huu”alisema Mkurugenzi huyo.
Aidha Nsonda alizungumzia kuhusu mwamko wa elimu katika Mji huo Makongolosi  na kusema kwamba zamani wazazi walikuwa wakiwatoa shule watoto kuwapeleka  machimbo ya dhahabu  lakini hivi sasa  kumekuwa na mwamko mkubwa wa kielimu..
Mkurugenzi huyo shule maarufu kwa jina la Baba Mzazi alisema kuwa hivi sasa kila mzazi katika Mji huo ana kiu ya kutaka kusomesha kutokana na kutambua umuhimu wa elimu hivi sasa.
Kwa upande wake Mwalimu anayefundisha darasa la kwanza katika shule hiyo, Tracila Joachim alisema katika kuwafundisha watoto amekuwa akitumia mbinu mbali mbali kama mwali ili watoto waweze kumwelewa  vizuri .
Mwisho.

No comments:

Post a comment