Friday, 7 February 2020

WANANCHI ARUSHA DC WATAKIWA KUENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI


Na. Elinipa Lupembe.
Wannchi wa Halmashauri ya Arusha, wametakiwa kuendelea kuunga mkono juhudi za kimaendeleo, zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano, inayo ongozwa na Dk John pombe Magufuli kwa kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta  za Elimu, Afya, Maji, kama adhma ya serikali ya kuelekea uchumi wa kati, ifikapo mwaka 2025.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha, Zelothe Stevene, wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha, ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka minne, tangu serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa, serikali ya awamu ya tano imefanya mabadiliko makubwa ya kimaendeleo nchini kwa kufanikiwa, kutekeleza miradi mingi kisekta, kwa muda mfupi, kulinganisha na awamu zilizotangulia, miradi ambayo imeleta mabadiliko makubwa kwa jamii, ususani wananchi waishio vijijini.
Amewapongeza wananchi wa vijiji vya Oldonywas, Mbuyuni na Nduruma kwa namna walivyo jitoa kuchangia nguvu zao, kutekeleza miradi ambayo serikali yao makini ilitoa fedha na wao kuchangia nguvu zao na kuwataka kuitunza miradi hiyo kwa faida yao na vizazi vijavyo.
"Nimeridhishwa sana na taarifa za miradi yote iliyotembelewa na Kamati yangu ya Siasa na kuona wananchi wakiwa wamechangia utekelezaji  wa miradi hiyo kwa zaidi ya asilimia 10, jambo ambalo miaka ya nyuma ilikuwa changamoto, hii inaonyesha wazi wananchi wametambua na kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano, amesema Mwenyekiti Steven"
Hata hivyo Mwenyekiti huyo, ameainisha miradi ya elimu na afya iliyotembelewa na kamati yake, ni pamoja na upanuzi wa Kituo cha Afya M'buyuni kata ya oljoro, uliogharimu shilingi milioni 400, upanuzi wa Kituo cha Kituo cha Afya Nduruma shilingi milioni 500 na ujenzi wa shule mpya ya Oldonyowas iliyo gharimu shilingi milioni 709.3.
Ameongeza kuwa vituo hivyo kwa sasa, vimeanza kutoa huduma sasa 24, ikiwa ni huduma ya kulaza, huduma ya upasuaji, huduma za kujifungua, maabara, pamoja na huduma za mama na mtoto, jambo ambalo litapunguza vifo visivyo vya lazima, hususani vifo vya mama na mtoto wakati wa  kujifungua, ikiwa ndio uhalisia wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Edward kivuyo ni mwananchi wa kijiji cha Mbuyuni, amesema kuwa wanajivunia maendeleo yaliyo letwa na Rais Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano, kwa kujenga kituo cha afya, kituo kilichowapunguzia adha ya kufuata huduma zaidi ya Kilomoira 40, adha ambayo ilisababisha wajawazito kujifungulia, nyumbani, wengine njiani wakienda hospitali, na wengine kupoteza maisha yao na watoto wao.
"Kituo hiki cha afya ni historia, hajawahi kutokea Oljoro, wanawake wengi walikua wanajifungulia nyumbani, wengine njiani kwa sababu ya umbali wa kituo cha afya,  tumepoteza kinamama na mtoto wakati wa kujifungua, lakini kwa sasa tunajivunia maendeleo  ya serikali yetu ya awamu ya tano kwa kutujengea kituo cha afya" amesema Kivuyo.
Kamati ya Siasa mkoa wa Arusha, imetembelea jumla ya miradi mikubwa mitatu yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6, ikiwa ni pamoja na ujenzi majengo ya Upasuaji, maabara, jengo la mama na mtoto, jengo la kuhifadhia maiti na nyumba ya mganga kituo cha Afya Nduruma, jengo la Upasuaji, maabara, jengo la mama na mtoto, nyumba ya mganga kituo cha Afya Mbuyuni, pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa, jengo la utawala, maabara za masomo ya sayansi, mabweni mawili ya wasichana na nyumba mbili za walimu, shule ya sekondari Oldonyowasi.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha, Zelothe Steven akikagua ujenzi wa maabara shule ya sekondari Oldonyowas.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha, Zelothe Steven akikagua ujenzi wa maabara shule ya sekondari Oldonyowas.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha, Zelothe Steven akikagua ujenzi wa maabara shule ya sekondari Oldonyowas.

No comments:

Post a comment