Sunday, 16 February 2020

UVCCM MBEYA YAZINDUA KAULI MBIU YA TUJENGE MATUMAINI YA PAMOJA


Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzu (UVCCM) Mkoa wa Mbeya wamefanya ziara katika Wilaya ya Chunya na kuzindua mpango mkakati wa Mkoa wa Mbeya unaoenda kwa jina la "Tujenge Matumaini ya Pamoja" wakishirikiana na Uvccm Mabinti wa Mkoa wa Mbeya ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mhe.Mkuu wa ya Wilaya Chunya Eng.Marryprisca Mahundi,Ambapo mpango mkakati wa Mkoa mzima ni kuzunguka Wilaya zote kutoa Elimu ya Afya,mazingira,maendeleo ya Mkoa wetu pamoja na darasa la Binti jitambue thamani yako ambapo waelimishaji wanatoa Elimu.


Pia ziara hiyo Wilaya ya Chunya ilienda na zoezi la kutoa misaada
(1) Gereza Chunya (2) Kituo cha Watoto yatima Chunya (3)baadhi ya Shule za Sekondari Wilaya ya Chunya.

Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti UVCCM mkoa Ndg. Mohamed Mashango akiwa na Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa,Viongozi wa idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Mbeya na wajumbe wa Kamati ndogondogo zote za UVCCM mkoa wa Mbeya.


No comments:

Post a comment