NA MWANDISHI WETU.

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ametoa zawadi mbalimbali kama motisha kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri ndani ya mkoa huo huku akitoa agizo wapewe kipaumbele wanapokwenda kwenye mahitahi haswa maeneo ya umma.

Mtaka kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii alibainisha kuwa:

"Tumewapongeza walimu wetu kwa kufaulisha vizuri na kuufanya mkoa wetu kuingia katika mikoa 10 bora katika mitihani yote ya kitaifa msingi na sekondari.

Tumemzawadia mwanafunzi aliyepata ufaulu wa daraja la kwanza point saba-Yohana Lameck Lugedenga (Tsh. Milion 1,(Mameneja wa Bank ya CRDB Tanzania-walimzawadia kijana wetu hundi yenye thamani ya Tsh.Milioni 2.2).

"Pia kwenye mitihani ya darasa la saba, wanafunzi wanne wa mkoa wa Simiyu waliingia kumi bora kitaifa kwa shule za serikali,kila mwanafunzi tumempa laki 3,tumewazawadia walimu wote ambao walipata Alama A kwenye masomo yao kidato cha nne.

kila A ya kidato cha nne Mwalimu amepata Tsh. elfu 30, Shule ya msingi ya Msingi Mwaukoli-Meatu iliingia 10 bora kitaifa kwa shule za serikali-Tumeizawadia Tsh. Milioni 2, shule 3 za msingi zilizoongeza ufaulu kwa miaka 3 mfululizo kila shule tumewazawadia Tsh.laki 5, shule 3 za msingi zilizoongoza kwa kuwa alama A nyingi katika kila somo zimepata zawadi za fedha, Nazipongeza Halmashauri zetu zote kwa kutenga fedha za motisha za elimu kwa walimu wote wa msingi na sekondari, nawapongeza wadau wote wa mkoa wa Simiyu, Bank za CRDB, NMB,TPB kwa mchango wao mkubwa katika kambi za kitaaluma mkoani kwetu "

".Zaidi ya yote, tumekubaliana walimu wetu wote ndani ya Mkoa ,kupewa kipaumbele cha kwanza wanapokwenda kwenye ofisi au taasisi za umma kupata huduma katika mantiki ya kwamba, Mwalimu anapokaa kwenye foleni kusubiri huduma, mamia ya wanafunzi wake darasani wana athirika kwa kupoteza kipindi kwa siku hiyo, hivyo mahala popote ambapo ofisi ya serikali inahusika (Hospitali ,Ofisi za Halmashauri, na maeneo mengine ya umma )Mwalimu akifika akajitambulisha kwa kitambulisho chake basi ahudumiwe haraka,ili aweze kurejea kwenye kituo chake cha kazi mapema,tumeyashauri Mabenki pia yaje na namna bora ya kuwasaidia mikopo midogo walimu ambao hawakopesheki baada ya kufikia ukomo wa kukopa kwa sheria ya BOT,ili kuwaondoa kwenye kadhia ya kukopeshwa na watu au taasisi binafsi ambazo zimegeuka kuwa mwiba kwa walimu kutokana na riba kubwa hali inayosababisha baadhi ya walimu wetu kushuka morali ya kufundisha na wengine kukwepa kwenda vituoni pao pa kazi kwa kuogopa kudaiwa."

"Tumewahakikishia walimu wetu kuendelea kuwalinda na kutunza utu na heshima yao, na kuwaomba viongozi wenzangu ndani ya mkoa kujiepusha na lugha au kauli za kuwakatisha tamaa, kejeli au vitisho".

"Nawapongeza, wazazi, walezi, sekta binafsi, viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa, watumishi wenzangu na walimu na wanafunzi wetu kwa kuibeba ajenda ya elimu kama kipaumbele cha kwanza." Alieleza RC Mtaka katika taarifa yake hiyo.

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: