Friday, 14 February 2020

SERIKALI YAKITEUWA CHUO CHA UALIMU MOROGORO KUFUNDISHA SOMO LA HISABATI

          Na Ahmed Mahmoud,Arusha
Serikali imekiteua chuo cha ualimu Morogoro kufundisha waaalimu wa Hisabati kwa lengo la kupunguza upungufu wa waalimu wa sayansi na Hisabati nchini ikiwa ni sehemu ya  mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu TESP.

Kwa muktadha huo chuo hicho kitatoa mafunzo kwa waalimu wa masomo ya Hisabati baada ya serikali kukiteua kufundisha waalimu tarajali na walipo kazini kuongeza ufanisi wa kufundisha somo hilo ambalo limekuwa na upungufu wa waalimu.

Hayo yameelezwa na Naibu katibu mkuu wa wizara ya Elimu sayansi na teknolojia Dkt.Avemaria Semakafu wakati wa mkutano mkuu wa kutafakari mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu TESP inayoendelea jijini Hapa.

Alisema kuwa serikali itatoa ajira 16,000 za ualimu ili kuondoa suala zima la upungufu wa waalimu hususani wa sayansi na hisabati huku malengo ya mradi huo ikiwa ni kuendeleza elimu ya ualimu kwa kutoa mafunzo kazini na kwa waalimu tarajali.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi wa Mkutano huo Katibu Tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega alisema ili nchi yeyote inayohitaji maendeleo endelevu  inahitaji kuwekeza kwenye sekta ya elimu kwa waalimu kutoa elimu yenye ubora wa hali ya juu na viwango Bora ambapo serikali ya awamu ya tano imeonyesha hilo kupitia mradi huo.

Alisema kuwa unapofika kwenye vyuo vya ualimu taswira imebadilika tofauti na hapo awali na kuwataka wakuu wa vyuo kutumia nafasi hiyo kutafakari changamoto na mafanikio kwenye mkutano huo kuongeza ubora katika kufundisha vijana kwa kuwa mazingira ya ufundishaji na kufundisha yameboreshwa.

Nae Kamishna wa Elimu Dkt.Lyabwene Mtahabwa  alisema kuwa nchi yoyote makini inayotaka maendeleo endelevu lazima iwekeze kwenye elimu hususani mafunzo ya ualimu kwa kuwaanda kwa ubora wenye viwango nasi ndio tumefikia huko kwa Sasa.

Alieleza kuwa fursa za upatikanaji wa elimu bila Upendo ni changamoto kwa kuwa ualimu bila Upendo kwa wanafunzi bado haotasaidoa kuzalisha wanafunzi wenye ubora katika sekta ya Elimu.

Mwisho.

No comments:

Post a comment