MbungewaJimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Danieli Mtuka aliyenyanyua mikono akitoa ufafanuzi kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula (mwenyemiwani) wakati alipotembelea kwenye mradi mkubwa washamba la pamoja la Korosho lenye zaidi ya ekari 12000 eneo la Masagati Manyoni Mkoani Singida leo kulia kwa Mangula ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Jackson Mwagisa (pichana John Mapepele)

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula akikagua Mkorosho kwenye mradi mkubwa wa shamba la pamoja la Korosho lenye zaidi ya ekari 12000 eneo la Masagati Manyoni Mkoani Singida leo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku saba katika Mkoa wa Singida(Pichana John Mapepele

      Makamu Mwenyekitiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania  Bara, Philipo Japhet Mangula akikata keki maalum ya miaka 43 ya Chama Cha Mapinduzi katika kikao cha tathmini na majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku saba mkoani Singida kwenye ukumbi wa maktaba wilayani Manyoni leo kulia ni Mwenyekitiwa CCM Mkoa wa Singida Alhaji Juma kilimba kushoto ni Mwenyekitiwa CCM Wilaya ya Manyoni Jumanne Mahanda anayefuata Katibu wa CCM Mkoa wa Singida AlexndrinaKatabi(Pichana John Mapepele)



    Umati wa wanachama wa CCM  uliohudhuria mkutano wa Makamu Mwenyekitiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula(Picha na John Mapepele)


Apongeza Mkoa wa Singida 

Na John Mapepele

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Philipo Japhet Mangula  amewataka watanzania kutochezea  amani  na  kuyumbishwa na wanasiasia  na badala yake  waione amani walio nayo kama mtaji mkubwa wa kuwaletea maendeleo ya kweli kwa kizazi cha sasa na baadaye.
Mangula ameyasema haya leo katika ukumbi wa maktaba Manyoni wakati alipohitimisha ziara yake ya kikazi ya siku saba kwenye Mkoa wa Singida ambapo amesema Tanzania  ni miongoni mwa nchi chache duniani ambayo imebahatika kuwa amani katika kipindi chote kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Alisema hivyo ni wajibu  wa kila mwananchi mzalendo  kuilinda kwa kuwa  watu wengi hawapendi kuona Tanzania  ina amani na kupiga maendeleo ya haraka kama inavyofanya sasa.
“Ndugu zangu hata tukichukulia mfano mdogo tu, katika kipindi cha miaka 75 ambayo tulitawaliwa na Wajerumani na Waingereza kwenye Wilaya yote ya Manyoni  hatukuwa hata na Shule mmoja ya Sekondari lakini  leo tuna zaidi ya shule 30 katika kipindi kifupi, je hayo siyo maendeleo makubwa ?” alihoji Mangula
Alisisitiza kuwa mapinduzi  makubwa  ya kiuchumi yanayofanywa  na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli yanatokana na  msingi  imara uliojengwa ambao ni amani na kwamba wachafuzi wa kubwa  wa amani dunani kote ni wanasiasa  ambao wamekuwa wakisukumwa na tamaa ya madaraka ambapo yakitokea  wanaoumia ni  watoto, wazee na akina mama.
Akitolea mfano wa machafuko ya kisiasa ya Rwanda ya mwaka 1994 alisema akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera wakati huo,  alishuhudia wimbi kubwa la watoto na akina mama wakiteseka  na kufa njiani wakati wakijaribu kukimbia nchi yao  kunuisuru maisha yao.
“Nilishuhudia  mama akina mama  wakitanda kanga na kumsaidia mama mwenzao kujifungua mtoto pembeni mwa barabara na baada ya kujifungua tu wakaendelea na  safari, kwa kweli  huwa sipendi kukumbuka  hali ile maana  ni  hatari na ukatili usioelezeka” aliongeza Mangula
Akiwa katika mkutano huo amesisitiza suala la uadilifu na kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za chama   cha Mapinduzi ambapo amesema vitendo vyoyote vya rushwa na wagombea kuanza kujipitisha kabla ya kipindi rasmi cha kuchukua fomu za kugombea na kuanza mchakato wa uchaguzi hakikubaliki na kusisitiza kuwa chama kitachukua hatua kwa wote watakao bainika kufanya hivyo.
Aidha Kamati za Siasa katika maeneo husika zitakazoshindwa kuwachukulia hatua wanachama watakaofanya makosa zitaadhibiwa.
Akiwa katika ziara hiyo ametembelea  miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Mkoa wa Singida ambapo mradi wa mwisho alioutembelea ni mradi mkubwa wa shamba la pamoja la Korosho lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 12000 eneo la Masagati kwenye Wilaya ya Manyoni na kusifu juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuleta mapinduzi makubwa  ya kilimo kwa wananchi bila kujali itikadi ya vyama vyao.
Amesema alama ya Chama Cha Mapinduzi ni jembe na nyundo ambapo amesema jembe ni alama ya mkulima  na nyundo ni mfanyakazi hivyo CCM inaamini kuwa  wakulima  na wafanyakazi wanamchango mkubwa katika kuchangia uchumi wa nchi yao na kuwa   mapinduzi ya uchumi hapa Tanzania yameletwa na kilimo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Danieli Mtuka akimwelezea Mangula kwenye shamba  la Korosho la Masagati ameshukuru Serikali ya Mkoa wa Singida chini ya Mkuu wa Mkoa, Dkt. Rehema Nchimbi kwa kushirikisha wananchi katika  kuwabadili  mawazo na mtazamo wa kutafuta maendeleo ya kweli  kwa kulima shamba la pamoja la korosho ambapo amesema wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Mhe. Mtuka amesema kutokana na utafiti uliofanyika  na watafiti wa kilimo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Mazao ya Kilimo Naliendele kwa kushirikiana na watafiti wa mazao ya Kilimo Kanda ya Kati uliofanyika  kuanzia mwaka  2002, matokeo ya utafiti huo yalionyesha  kuwa hali ya hewa na udongo vinafaa kwa kilimo cha korosho hivyo wakaanza kuwahamashisha wananchi kulima zao hilo
“ Kwa kushirikiana na Uongozi wa Mkoa na Halmashauri tuliamua kuanzisha zao la korosho kimkakati ili kuchochea kwa kasi kubwa  ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja wilaya,mkoa  na taifa kwa ujumla’” aliongeza Mhe. Mtuka
Aidha,alipongeza  Serikali ya Mkoa kwa kubuni wazo la kuanzishwa kituo kwa kikubwa cha  hija duniani cha Bikira Maria  katika eneo la Sukamahela, sehemu ambayo ni katikati ya nchi ya Tanzania  kwa ajili ya watu kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuhiji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Charles Fussi amesema kuwa kazi  zinazoendelea katika eneo hilo kwa sasa  ni  kuhamasisha wakulima  wajiunge na kilimo cha korosho, kuendelea kutoa huduma za ugani kwa wakulima ikiwa ni pamoja na  matumizi sahihi ya viuatilifu kwa kushirikiana na TARI na Bodi ya Korosho, kuendelea kazi ya kusafisha na kugawa mashamba kwa wakulima na kuzalisha miche  bora  korosho.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Rahabu Jackson Mwagisa  amemhakikishia Mangula kuwa serikali itaendelea  kusimamia kikamilifu  na kuwa hamasisha wananchi kutoka sehemu mbali mbali nchini  kuja kuwekeza katika  kilimo  cha korosho kwenye eneo hilo kwa kuwa mradi huo na manufaa makubwa kwa wananchi wa wilaya  ya Manyoni na Taifa kwa ujumla.
Ametaja baadhi ya manufaa ya mradi huo kuwa ni pamoja na  udhibiti wa  visumbufu kama magonjwa na wadudu,udhibiti wa  ubora wa korosho kutokana na usimamizi wa karibu, upatikanaji wa uhakika wa soko katika eneo la mradi,kurahisisha upatikanaji wa pembejeo na huduma za ugani ili kuhudumia eneo kubwa kwa wakati mmoja na chanzo kikuu  cha malighafi za viwanda vya kusindika korosho.
Manufaa mengine ya mradi ni kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri kupitia ushuru na kodi za biashara mbalimbali zitokanazo na ongezeko la uchumi katika sekta mtambuka zinazoendana na zao hilo, hali ya maisha  kuboreka ikiwa ni  pamoja na ujenzi wa makazi bora na kuongezeka  uhakika  wa chakula  katika kaya.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: