Wednesday, 26 February 2020

EWURA YACHARUKA NA KUSEMA WAUZAJI WA MITUNGI YA GESI BILA MIZANI FAINI MILIONI 3.Meneja  Mawasiliano na Uhusiano  EWURA Bw.Titus Kaguo

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Wananchi katika maeneo mbalimbali jijini Dodoma wamelalamika kutokana na wauzaji wa mitungi ya gesi kuendelea kuuza mitungi hiyo bila kupimwa kwenye mizani hali ambayo husababisha kuuziwa mitungi isiyokuwa na uzito uliosahihi.
Wakizungumza na    mtandao baadhi ya wananchi hao ambao majina yao yamehifadhiwa wasema kuwa  kitendo cha kuuziwa au kubadilishiwa mitungi ya gesi bila kupimwa imekuwa changamoto kubwa kwao kwani hali hiyo wakati mwingine husababisha kununua mitungi isiyokuwa na ujazo usio sahihi na kusababisha gesi kuisha mapema.
“Mawakala wa gesi wanatakiwa wawe wana  mizani  ya kupimia mitungi ya gesi kwa sababu kuna wizi mkubwa mtu unaenda kununua mtungi wa gesi  unakuta upo nusu ama robo unaisha hata mwezi haujaisha “walisema.
Kutokana na changamoto hiyo wameziomba Mamlaka zinazohusika ikiwemo EWURA kulifuatilia kwa umakini suala hilo ili kuondoa usumbufu huo huku pia wakilalamikia kwa gesi kuendelea kupanda kila kukicha.

Kwa upande wake  Meneja Mawasiliano na Uhusiano Mamlaka ya udhibiti  wa nishati,na maji  hapa nchini [EWURA] Bw.Titus Kaguo akizungumza na mtandao huu amesema   adhabu kwa mtu anayeuza mitungi ya gesi bila mzani ni milioni tatu  na changamoto iliyopo ni uelewa mdogo.
“Hii ni bidhaa ambayo si ya muda mrefu sana na sheria mtu anapouza mtungi wa gesi bila mzani adhabu yake ni milioni 3 hivyo unaweza ukakuta  unafunga vibanda vyote vya kuuzia mitungi ya gesi na kinachotakiwa sasa ni uelewa kwa wananchi”amesema.

Kuhusu kupanda kwa bei ya gesi  Bw.Kaguo alisema huwa kuna vigezo maalum na pindi makampuni ya gesi yanapopandisha bei huitwa na Mamlaka hiyo kuhojiwa sababu za kupandisha bidhaa hiyo.
Hata hivyo,Bw.Kaguo alisema mafunzo  kwa wadau wa gesi yanaendelea katika maeneo mbalimbali nchini  ili kuwanoa zaidi namna  ya matumizi bora ya gesi na kuachana na kutumia kuni na mkaa.
Hata hivyo ,mtandao huu umeweza kuzungumza na mmoja wa Mawaka wa mitungi ya ya gesi  ambaye hakutaka jina lake kuandikwa kwenye gazeti ambapo alisema yeye kama mfanyabiashara anashindwa kumudu gharama za mzani kulingana na biashara yake huku akisema kupanda kwa bei ya gesi inatokana na kupanda kwa gharama za maisha.

No comments:

Post a comment