Pichani ni Mratibu na Mkurugenzi wa mbio za Kilimarathon John Bayo


  Na Vero Ignatus,Arusha.

Tahadhari imetolewa kwa wakimbiaji wa mbio za KiliMarathoni ambao wanatumia namba zilizokwisha kutumika miaka iliyopita kuacha mara moja kwani jambo hilo halitafungiwa macho bali  sheria itachukua mkondo wake.

Akizungumza  Mratibu na Mkurugenzi wa mbio hizo John Bayo alisema kuwa tabia hiyo siyo njema kwani inawanawanyima huduma wale wote  waliolipia namba hizo kwaajili ya mbio 2020

‘’Mwaka jana tulipata watu waliokimbia na namba za miaka iliyopita kuna wengine walikimbia bila namba za km5 kwa kukosa namba za km 21 ukikosa nakuomba utulie ili usijekusumbuliwa na askari’’

Amesema kuwa awali wakati wa uzinduzi waandaaji walitoa taarifa  kuwa mbio za full Marathon km 42 itakuwa na watu 800 ile ya Kilimanjaro premium lager itakuwa na watu 800 tigo half marathon ikiwa na watu 5500

Aidha kuhusu suala la usalama Bayo alisema kuwa wamejipanga na wamejaribu kuweka idadi isizidi kwasababu barabara ni nyembamba ili kuepusha hatari ya msongamano, kwa upande wa Afya tayari wameshaandaa timu ya madaktari kutoka hospitali za Kcmc,Mawezi, kwaajili ya kuwahudumia wakimbiaji pia kutakuwepo na Ambulace 8 na kila moja wapo itakuwa na polisi na radio kwaajili ya kutoa taarifa kama kutakuwa na tukio lolote

Alisema kuwa tayari wameshaandaa watu katika maeneo tofautitofauti likiwemo jeshi la polisi kwaajili ya kuwaangalia watu ambao hawana namba ili kuchukuliwa hatua za kisheria 

Aidha Wanariadha wanaotoka nje ya Tanzania wapo zaidi ya nchi 53 ambao watashiriki  katika mbio za Kilimarathon,washiriki wanatarajiwa kuwa 11,000,ambapo kwa upande wa Tanzania wakimbiaji wote wa kitaifa tayari wameshaingia isipokuwa Emanuel Giniki atakuwa na mbio nje ya nchi wiki ijayo hivyo hataweza kushiriki.

 Bayo amesema kuwa leo kwa wakazi wa Jiji la Arusha ni siku ambayo namba zimetolewa kwaajili ya kujisajili kwaajili yam bio za km tano,wale wote ambao watakimbia km21 na km42 wote hawa namba zinatolewa siku ya leo 25 na kesho tar 26 katika hotel ya Kibo Palace pamoja na wale wa km 5 pia usajili unaendelea hapo kesho Tarehe 26/3/2020.

Mwisho

Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: