Afisa uhusiano wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Angela Mziray akifafanua  baadhi ya maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi katika kikao kazi cha kuwapa elimu juu ya vifurushi vipya pamoja na huduma za mfuko huo

Waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigom kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye kikao kazi na watendaji wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)
Rais wa umoja wa vyama vya habari Tanzania(UTPC)Deogratius Nsokolo akichangia katika kikao kazi cha waandishi wa Kigoma na watendaji wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)
........................................................
Na Editha Karlo,Kigoma
MFuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)leo umekutana na waandishi wa habari wa  Mkoa wa Kigoma ikiwa ni utekelezaji wa mpango wake wa kuelimisha umma juu ya mpango wa vifurushi vya bima ya afya na huduma zitolewazo na mfuko huo.

Akifungua kikao hicho, mkurugenzi Mkuu wa mfuko Bw. Bernard Konga  amesema kuwa, alma ya Mfuko ni kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha na wanachukua hatua ya kujiunga ili kuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu.

Akifafanua baadhi ya hoja zilizoibuliwa katika kikao hicho, Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja Bwana Hipoliti Lello ametoa wito kwa kundi la wanahabari  kujiunga na huduma za Mfuko kupitia vyama vyao vya waandishi wa habari.

Je kuna utofauti gani kati ya Kifurushi kimoja na kifurushi kingine?

Deogratius Nsokolo ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Kigoma, anaushukuru Mfuko kwa kuandaa utaratibu mzuri utakaowezesha wananchi na waandishi wa habari kunufaika na mpango huu.
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: