Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Agustivo iliyopo Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma 

Mwonekano wa shule 
Mkuu wa shule 

  Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Agustivo iliyopo Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wakipokea maagizo kutoka kwa walimu wao ambao hawapo pichani .PICHA ZOTE NA AMON MTEGA
......................................


WANAFUNZI wa shule ya Sekondari ya Agustivo iliyopo Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wameipongeza shule hiyo kwa kuwafundisha kwa vitendo somo la stadi za kazi mwandishi Amon Mtega anaripoti toka Ruvuma.

Akizungumza na Msumba News mmoja wa wanafunzi hao Agnes Mbawala amesema kuwa elimu hiyo inawapa mwanga namna  ya kujitegemea  pindi wanapohitimu elimu ya Sekondari na Vyuo.

Agnes ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha sita amesema kuwa licha ya kujitegemea lakini bado itaongeza ufanisi wa wanafunzi kuwa wabunifu kwa kujiajili wenyewe jambo ambalo litasaidia  kupunguza tatizo la ajira.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Moses Mapunda amesema kuwa shule hiyo ambayo inayoanzia na kitado cha kwanza hadi cha sita ,inamilikiwa na sekta binafsi imekuwa ikitoa elimu hiyo kwa vitendo ambayo imewafanya wanafunzi wanaohitimu hapo kuwa wachapakazi na wenyekujitambua.

 Mapunda amesema kuwa inashangaza baadhi ya Wanafunzi wanahitimu elimu zao hadi  ngazi ya vyuo lakini wamekuwa hawawezi kufanya shughuli za mikono ambazo zina nafasi kubwa ya kuwafanya waweze kujitegemea na kuacha kuwa tegemezi kwenye maisha.

 Akizitaja baadhi ya elimu inayofanywa kwa njia ya vitendo kuwa ni ufugaji wa mifugo mbalimbali ulimaji wa bustani ambapo mwanafunzi anafundishwa namana  upangaji wa matuta kulingana na zao linalotakiwa lipandwe.

 Amesema kuwa licha ya kufundisha elimu ya vitendo  lakini bado shule hiyo imekuwa ikitoa elimu ya utunzaji wa mazingira ambayo itawasaidiwa wanafunzi pindi wanapohitimu waende wakaielimishe jamii namna ya umhimu wa utunzaji wa mazingira ili yasiharibiwe ovyo.

 Katika suala la kuboresha mazingira mkuu huyo amesema shule inasehemu yenye chanzo cha maji ambacho kimekuwa ni moja ya sehemu ya kufundishia jinsi ya kuvilinda vyanzo vya maji viharibiwe.

 Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa chanzo hicho lakini bado shule hiyo inashamba la miti ambalo wanafunzi hujifunzia namna ya upandaji miti pamoja na kuianisha kitalaamu kwa kuzingatia hali ya hewa ya maeneo husika.

  Mkuu huyo akizungumzia suala la taaluma kwa ujumla amesema kuwa shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani yake ambapo katika kipindi cha msimu uliopita kwa wanafunzi wa kidato cha Nne kati ya wanafunzi 69 walifaulisha  daraja la kwanza  sita,daraja la pili 35 ,daraja la tatu 20 na daraja la nne ni nane huku waliofeli hawakuwepo.

Kwa  kidato cha sita amesema wahitimu walikuwa 33 na kuwa daraja la kwanza walikuwa 10 ,daraja la pili 20 ,na daraja la tatu walikuwa watatu huku daraja la nne hawakuwepo.

  Aidha shule hiyo inafundisha pia masomo ya kutumia Computer  ambapo wanafunzi wote wamekuwa wakipata furusa hiyo ambayo inawawesha hata kutambua nini maana ya Tehama.

 Mwalimu wa Computer Lucida Ndunguru amesema kuwa wanafunzi wote wamekuwa wakipata fursa ya kujifunza ambapo hadi sasa wengi wao tayari wanamudu vizuri kutumia computer.

 Hata hivyo amesema changamoto kubwa ni pale umeme unapokuwa umekatika wakati wanafunzi wapo kwenye somo la namna ya utumiaji wa computer  .

                         MWISHO.
.
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: