MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na UJUMBE wa Wabunge kutoka nchini Finland wametua nchini kwa ziara yao ya siku tatu mkoani Tanga na Visiwani Zanzibar ambapo watatembelea miradi inayofadhiliwa na Serikali ya Finland.
Mmoja wa Wabunge wa nchini Finland kushoto akitate jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella leo mara baada ya kumtembelea ofisini kwake katikati ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
 Mmoja wa wabunge hao akimuuliza swali mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella ambaye hayupo pichani
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akiwa na mmoja wa wabunge kutoka nchini Finland kulia wakiteta jambo

 MKUU wa Mkoa wa Tanga akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe huo mara baada ya kuzungumza nao
 Sehemu ya ujumbe wa Wabunge kutoka nchini Finland wakiingia kwenye Kituo cha Kulea Watoto wenye ulemavu cha (YDCP) Jijini Tanga wakiongozwa na Mratibu wa Kituo hicho Leopodi Abeid kushoto aliyevaa suti nyeusi
 Mratibu wa Kituo hicho Leopodi Abeid akiwaongoza ujumbe huo kuingia kwenye kituo hicho
Mmoja wa wajumbe hao wakisaini kitabu cha wageni kwenye kituo hicho mara baada ya kukitembelea
 Ujumbe huo wakipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa mambo mbalimbali kwenye kituo hicho

UJUMBE wa Wabunge kutoka nchini Finland wametua nchini kwa ziara yao ya siku tatu mkoani Tanga na Visiwani Zanzibar ambapo watatembelea miradi inayofadhiliwa na Serikali ya Finland.
 

Miradi ambayo watatembelea ni kwenye maendeleo ya Jamii, miradi ya watu wenye ulemavu  jinsi ya kuwasaidia ili waweze kujiingiza kwenye shughuli za kimaendeleo na hatimaye kuweza kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza wakati ujumbe huo ulipokwenda kukutana naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella aliwashukuru kwa kuchagua kutembelea mkoa huo kwa sababu hapa nchini kuna mikoa mingi.

Mkuu huyo wa mkoa aliwaambia ujumbe huo kwamba mkoa huo ni miongoni mwa mikoa inayozalisha kilimo cha Korosho Matunda na Mkonge ambapo kwa asilimia kubwa mkonge unapatikana mkoani hapa hivyo wanaweza kwenda kuiona ili waweze kuwa mabalozi wazuri.

Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba mkoa huo unazalisha matunda kwa wingi na hivi sasa wanatengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji kuja kuwekeza viwanda vya matunda kwa kufanya uzalishaji ambao utakuwa na tija kwa wakulima.

“Kwa sasa wakulima wanazalisha kiasi kikubwa cha matunda lakini tunapata soko dogo kutokana kutokuwepo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kukosekana kwa viwanda hivyo ninaamini kwamba aina hii ya mahusiano itakuwa na tija siku za mbeleni”Alisema

“Lakini pia niwaambie kwamba wananchi wa mkoa wa Tanga ni wakarimu sana hivyo mnaweza kuwashawishi wawekezaji kwenye maeneo mnayotoka wakaja kuwekeza kwani kuna mazingira rafiki kwa uwekazaji”Alisema

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa alikishukuru kituo cha Kulea Watoto wenye ulemavu cha (YDCP) kutokana na kuona namna nzuri ya kuhakikisha watu wenye ulemavu wapata elimu na hivyo kuweza kujitegemea.

“lakini pia tunawashukuru FIDA kwa msaada wenu kwa kuwasaidia watoto hao na kuwaonyesha namna mnavyowajali vijana hao kwani umewasaidia watoto wanatoka kwenye mazingira magumu kuweza kupata elimu kutokana na ukata unaozikabili familia zao hivyo sisi kama serikali tunashukuru sana”Alisema RC Shigella.

RC Shigella alisema kwa sasa serikali inatengeneza mazingira mazuri ya kuwawezesha ofisi zote za umma zinakuwa mazingira wewezeshi kwa watu wenye ulemavu.

“Mtazamo wa watu wa Tanga kuhusu watu wenye ulemavu umebadilika hivi sasa kutokana na kazi kubwa inayofanywa na FIDA,Kanisa na kituo cha YDCP tunashukuru tutaendelea na ushirikiano huo na utakuwa mzuri na tunashukuru na kutambua mchango wetu”Alisema

Awali akizungumza Mratibu wa Kituo cha YDCP Leopodi Abeid leo wamepokea wageni kutoka Finland ni marafiki wa kanisa la FCT wanaosaidia katika miradi mbalimbali hapo Tanga wanasaidia kituo cha watoto walemavu kutoka mwaka 2006.

Alisema kwamba serikali ya Finland wamewatuma wabunge hao kuja kujionea kwa macho shughuli zinafanyika hapa nchini na watazunguka kwenye miradi yote na watapata taarifa za miradi hiyo ili watakaporudi waweze kuwasilisha walichokiona.

Mratibu huyo alisema kwamba katika msafara huo wamekuja wawakikishi wa wabunge wenzao wamekuja wanne ambao wameambatana na Afisa Mshauri wa miradi ya FIDA kwa ukanda wa East Afrika anakaa Nairobi.

Hata hivyo alisema pia kwenye msafara huo wapo pia Afisa kutoka Konga, Mshauri na Meneja wa Mradi Tanzania ambaye yupo Arusha wameandamana na Afisa miradi FCT makao makuu Mchungaji Jackson Muna na Afisa wa Mambo ya Afya na hedhi salama Jackson Senyu kutoa Fida Arusha.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: