KAMPENI ya Tumeboresha Sekta ya Afya inayoendeshwa na maafisa habari na mahusiano wa wizara ya afya na taasisi zake imeweza kushuhudia maboresho mbalimbali yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John  Joseph Magufuli huku ufanisi ukiongezeka maradufu mwandishi Andrew Chale anaripoti 

Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya dawa na vifaa tiba Tanzania (TMDA), Adam Fimbo hivi karibuni alipotembelewa na Maofisa habari hao pamoja na wanahabari wadau kutoka vyombo mbalimbali hapa nchini, aliweka wazi kuwa taasisi yake imepiga hatua na imekuwa ikipokea Watendaji kutoka mataifa mengine 11 kutoka barani Afrika  kuja kujifunza.

Fimbo alisema watendaji hao wamekuja Nchini kutokana na  maboresho sekta ya afya na  namna
bora ya kuimarisha mifumo ya udhibiti wa bidhaa hizo unavyofanywa na taasisi yake..

Fimbo ameeleza kuwa hatua ya WHO kuitambua mifumo ya TMDA imeifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Barani Afrika kufikia hatua hiyo.

"Tanzania ndiyo nchi pekee Barani Afrika ambayo imetambuliwa na
Shirika la afya duniani (WHO) kufikia ngazi ya tatu (Maturity
Level 3) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa." Alisema Fimbo.

Fimbo alisema kuwa, hatua hiyo ilitambuliwa mnamo mwaka 2018, tangu hapo wakawa wanapokea watendaji kutoka taasisi
mbalimbali za udhibiti barani Afrika ambao wamekuwa wakija nchini
kujifunza.


Aliongeza kuwa, ngazi ya juu iliyobaki ni ile ya level 4 ambapo wanazidi
kuimarisha mifumo yao kuweza kufikia ngazi hiyo ya ubora duniani.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2015/16 hadi 2018/19 amlaka
hiyo imefanikiwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea katika
utekelezaji wa mipango kazi yake.

"Katika kipindi cha 2019/20 Mamlaka itaendelea kutoa
kipaumbele katika utekezaji kwa ufanisi wa malengo mahususi
manane yaliyomo katika mpango mkakati wake wa miaka mitano
(2017/18 hadi 2021/22 ili pamoja na kufikia na kutimiza matarajio
ya wateja, pia kuweza kuendelea kulinda afya ya jamii,” alisema Fimbo.


Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: