Friday, 3 January 2020

MBUNGE BONAH AWAKIKISHIA WANAFUNZI WOTE KUSOMA

Mbunge wa Segerea  Bonah Ladslasu wa tatu kulia akiwa na viongozi mbali mbali
Mbunge wa Segerea  Bonah Ladslasu akizungumza na Wanafunzi wa kidato cha kwanza sekondari ya Bonyokwa manispaa  ya Ilala Leo ambapo Mh,Bonah alisema wanafunzi wote waliofaulu watakwenda shule 
NA HERI SHAABAN
MBUNGE wa Segerea (CCM) Bonah Ladslaus amesema wanafunzi wa kidato cha kwanza waliofaulu mwaka huu katika jimbo la Segerea  wataanza Shule .

Mbunge  Bonah aliyasema hayo katika ziara yake endelevu ya sekta ya elimu ambayo ilikuwa ikikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na Shule mpya zilizojengwa katika uongozi wake ..


" Ndani ya Jimbo langu la Segerea    sekta ya elimu katika kumuunga mkono Rais John Magufuli nimesimamia shule 16 za sekondari  mpaka sasa na zote wanafunzi watasoma kuanzia jumatatu " alisema Bonah

Bonah alizitaja shule hizo za sekondari Bonyokwa,Kisukuru,Segerea Shule mbili,Buguruni moja,Kiwalani moja ,Kipawa mbili ,Kinyerezi Shule nne ,Vingunguti moja,Tabata moja,Kimanga moja.

Aliwataka wazazi kuzingatia elimu na kushirikiana na Walimu katika kukuza taaluma .

Katika ziara hiyo Mbunge Bonah alitembelea  Tabata  ,Kiwalani,Buguruni, Kipawa,Mnyamani,Kinyerezi,Bonyokwa ,ambapo katika Kata ya Tabata  Barbara ya Umoja road inakabidhiwa Mkandarasi January 02/2020 Barabara ya Tabata Kisiwani nayo inakabidhiwa Mkandarasi January  02/2020.

Akizungumza katika ziara hiyo mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala jumanne  Shauri alisema Kata ya Mnyamani amemkabidhi mhandisi wa Manispaa  ya Ilala kufanya tathimini kwa ajili ya mitaro mtaa wa faru kuelekea viwanja vya Sinai..


Shauri alisema Watendaji wake kuanzia jumatatu watakuwepo eneo hilo kwa ajili ya kushughulikia kazi hiyo ili kuwanusuru wananchi kwa mvua za mafuriko.


No comments:

Post a comment