Mkurugenzi wa Huduma Za Maabara wa TMDA, Dkt. Danstan Hipolite akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya TMDA waliotembelea Maabara hiyo ya Kanda ya Ziwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya TMDA,  Balozi, Dkt. Ben Moses (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi hiyo.


Katika kuendelea kuboresha huduma za afya nchini ,bodi  ya ushauri ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(MAB) imefanya  ziara maalum na kujionea mambo mbalimbali ya utendaji kazi katika ofisi ya Kanda ya Ziwa ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA).

Kupitia ziara hiyo bodi  imeweza kujionea utendaji kazi za udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika maabara kubwa nacya kisasa  iliyojengwa kanda ya Ziwa jijini Mwanza kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.

Aidha, bodi hiyo imeweza kufanya kikao chake  cha kawaida, ikiwa ni cha kwanza kwa mwaka 2020.

Pamoja na hilo bodi imekutana na watumishi wa TMDA kanda ya Ziwa ambapo Mwenyekiti wa MAB, Mhe. Balozi, Dkt. Ben Moses amewapongeza Menejimenti naxwatumishi kwa mafanikio ya utendaji kazi yaliyofikiwa na kuwahimiza kuendelea kujituma na kufanya kazi kwa weledi zaidi ili kuwezesha taasisi kufikia lengo lake la kuendelea kulinda afya ya wananchi kwa ufanisi zaidi.

Ziara ya wajumbe wa MAB inahusisha pia kutembelea na kujionea changamoto za udhibiti katika vituo vya Forodha vya Sirari na Mutukula.

Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: