Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Walemavu wenye kipato cha chini waishio katika maeneo ya vijijini wameomba kupatiwa bima ya afya ili kupata matibabu ya uhakika na kunusuru maisha yao  kutokana na wengi wao kusumbuliwa na magonjwa ya muda mrefu.
Wakizungumza  katika maadhimisho ya siku ya  walemavu,walemavu hao Mathayo Lengasha  wamesema kuwa wamekua wakipata shida hususan walemavu wa ngozi ambao wamekua wakisumbuliwa na saratani ya ngozi ambapo wameomba kupatiwa mafuta ya ngozi na bima ili waweze kutibiwa.
Mwenyekiti wa Shirikikisho la Vyama vya Walemavu katika Wilaya ya Monduli  Dorah Msuya amesema kuwa licha ya serikali kutoa maelekezo ya walemavu kutibiwa bila malipo bado ahadi hiyo haitekelezwi hivyo ameitaka serikali kutoa bima kwa walemavu.
Hata hivyo Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Monduli Henrich Laizer  pamoja na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Monduli  ambaye ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Noelia Myonga wamesema kuwa serikali itaendelea kuhakikisha kuwa walemavu wanapata haki zao ikiwemo ya matibabu kupitia sera na sheria mbalimbali zilizopo nchini.
Wilaya ya Monduli inakadiriwa kuwa na walemavu 672 ambao ni walemavu wa viungo,walemavu wa ngozi pamoja na walemavu wa akili.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: