Saturday, 14 December 2019

MBUNGE TWEVE NA KOMBA WAIPA HESHIMA TANZANIA


Mbunge Rose Tweve akishangiliwa na wabunge wenzake 
Mbunge Rose Tweve  na Yosepher Komba kulia wakijiandaa kwa kuanza riadha 
Mbunge Rose Tweve kulia akiwakimbiza wakenya 
Wabunge wanaume wanamichezo toka Tanzania wakimshangilia mbunge Tweve
 Wabunge wanawake Rose Tweve na Yosepher Komba wameendelea kuing'aza nyota ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuibuka na medali za dhahabu katika mbio za mita Mia moja (100m) na mita elfu moja na Mia tano (1500m).

Wakati Rose Tweve kutoka Mkoa wa Iringa akiwaburuza wabunge wa nchi za Kenya, Uganda, Burundi na wale wa Bunge la Afrika Mashariki EALA,  Yosepher Komba kutoka Viti Maalum Mkoa wa Tanga aliwagaragaza wapinzani wake katika mbio za mita 1500.

Wabunge Hao Vijana sasa mwaka wa Pili mfululizo wanaendelea kuipeperusha vema Bendera ya Tanzania katika mchezo wa riadha Naendelea wanatarajia kuendelea tena hapo jumapili katika mbio za kupokezana Vijiji.

Kwa upande mwengine mwanamama Anatropia Teonest alimaliza nafasi ya Pili katika mbio za mita 400, huku wanaume kupokezana Vijiji Tanzania ilishika nafasi ya tatu.

Michezo hiyo inaendelea Kesho katika mchezo wa Wavu wanaume na wanawake wakati Bunge la Tanzania watajitupa uwanjani kuvaana na Bunge la Afrika Mashariki

No comments:

Post a comment