Thursday, 5 December 2019

VIJANA ZAIDI YA 200 KUADHIMISHO SIKU YA AFRIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJAROVijana Zaidi ya 200 kutoka nchi 55 za Afrika wanatarajia kupanda mlima Killimanjaro May 25 mwaka 2020 na kufika katika kilele cha mlima huo kama njia mojawapo ya maadhimisho ya Umoja wa Afrika  na Agenda 2063 za Afrika tunayoitaka.MWANDISHI FERDINnd SHAYO ANARIPOTI TOKA ARUSHA

Waratibu wa Safari  hiyo kutoka nchi za Zimbabwe,Tazania na Uganda wamesema kuwa ziara hiyo inalenga kuhamasisha utalii wa ndani katika nchi za Afrika na kuwataka Vijana kujitokeza kwa wingi katika kuungana na vijana wa Afrika kupanda mlima huo unaongoza kwa urefu barani Afrika na wa pili kwa dunia nzima.

Emanuel Motta ni mratibu  kutoka nchini Tanzania anasema kuwa maadhimisho ya umoja wa Afrika May 25 mwaka 2020 yatafanyika katika kilele cha mlima Kilimanjaro ambapo vijana watapeleka agenda 2063 za Afrika tunayoitaka pamoja na Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa

Mdau wa Masuala ya Vijana kutoka nchini Uganda,  Ayaa Musuya amesema kuwa kabla ya kupanda mlima huo kutakua na mashindano ya sanaa ya kuchora Afrika tunayoitaka na washindi watapata nafasi ya kupanda  mlima huo na kupeleka sanaa zao kileleni.

Kwa upande wake mratibu wa Ziara hiyo kutoka nchini Zimbabwe Munyaradzi Muzenda amesema kuwa watakuwa na mabango makubwa ya Afrika Tunaoitaka pamoja na  Agenda 2063 ya Afrika tunayoitaka ambayo yatabebwa na vijana ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana kutimiza ndoto zao

No comments:

Post a comment