Picha N0,1-3,Mkurugenzi  Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi Tume ya Taifa ,Dorothea Chale akizungumza na watumishi wa mkoani Ruvuma watakao tumika na ujazaji wa taarifa za Watu watakao jiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga Kura ambapo zoezi hilo litafanyika Desemba 30 mwaka huu na kuishia Januari tano 2020.
Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakifuatilia maelekezo 

  WATUMISHI  watakao tumika katika uandikishaji na uhakiki wa taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura mkoani Ruvuma wamepatiwa mafunzo yatakayowawezesha kuhakiki taarifa hizo .Mwandishi wetu Amon Mtega anaripoti toka Ruvuma

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa  mafunzo hayo mkurugenzi msaidizi idara ya dsimamizi wa uchaguzi tume ya taifa Dorothea Chale alisema kuwa idara hiyo imeamua kuwapa mafunzo waandikishaji hao ili wakaziweke kumbukumbu sahihi za watu ambao watakaokuwa wanaenda kujiandikisha kwenye daftari hilo.

  Chale amesema kuwa mfumo wa kuhakiki taarifa hizo pamoja na kuwaandikisha wapiga Kura wapya utatumika wa kisasa ambao tahusisha mashine za Kilekitroniki (BVR)ambazo zenye uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu zote za mwananchi.

    Akielezea waandikishaji waliopata mafunzo hayo ya uboreshaji wa daftari la mpiga Kura ni wakutoka Halmashauri zote za mkoani Ruvuma ambao  ni Maafisa uandikishaji ngazi ya jimbo ,Wasaidizi pamoja na watalaamu wa tehema ambao watakaokuwa wanashughulika na mashine za BVR ikiwemo kuzishughulikia changamoto zote.

   Aidha mkurugenzi huyo amewataka watalaamu hao waliopatiwa mafunzo waache kufanya kazi kwa mazoea kwani watambue kuwa mazingira yanabadilika kila wakati.

 “Kumekuwepo kwa baadhi yenu ambao walishawai kupatiwa mafunzo hayo katika siku za nyuma hivyo wanaweza kwenda kufanya kazi hiyo kimazoea jambo ambalo halitakiwi “amesema Mkurugenzi huyo msaidizi wa Idara ya usimamizi Tume ya Uchaguzi “Dorothea Chale.

   Zoezi la Uboreshaji wa daftari la mpiga Kura litaanza disemba 30 mwaka huu na litaishia Januari tano mwaka 2020 huku walingwa ni wapiga Kura wapya wenye sifa ,Waliopoteza vitambolisho vyao,Waliobadilisha makazi ya kuishi na waliokosea majina yao,ambao watapata fursa ya kupiga Kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: