Mkurugenzi wa jiji la Arusha akikagua madawati hayo .
Mkurugenzi wa jiji la Arusha ,Dokta Maulid Madeni akionyesha madawati hayo yaliyokabithiwa kwa Afisa elimu sekondari jiji la Arusha kwa ajili ya maandalizi ya wanafunzi wa  kidato Kwanza  hapo mwakani. 


Halmashauri ya jiji la Arusha imekabidhi jumla ya madawati 1,000 kwa afisa elimu wa sekondari jiji kwa ajili ya maandalizi ya wanafunzi wanaotarajiwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2020. 

Aidha halmashauri hiyo inaendelea kutengeneza madawati mengine 2,500 ambayo hadi ifikapo januari 3 mwakani yanatarajiwa kukamilika na kusambazwa katika shule zote za sekondari zenye uhitaji na upungufu wa madawati hayo. 

Akiongea wakati wa kukabidhi madawati hayo Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha ,Dokta Maulid Madeni alisema kuwa, halmashauri ya jiji ilikuwa na upungufu wa madawati ndipo wakaamua kutengeneza madawati wenyewe katika karakana yao ya jiji iliyopo katika shule ya msingi Kaloleni , ambapo walijipanga kutengeneza madawati 3,900 na hii ni kwa ajili ya shule zote za sekondari za jiji la Arusha 

“ndani ya halmashauri yetu hatutaki kuona wanafunzi wanakaa chini ,hawana madawati na ndio maana tumeamua kutengeneza wenyewe madawati haya ili wanafunzi ambao wanaingia mwakani wapate huduma nzuri na waweze kusoma vyema na kama mnavyoona ndugu waandishi, madawati yetu ni imara kabisa na yametengenezwa kwa kiwango cha juu ambacho sisi wenyewe ndio tumemuelekeza mkandarasi anaetengeza jinsi tunavyotaka “alisema Madeni 

Aliongeza kuwa, ili mwanafunzi aweze kufaulu vyema ni lazima mazingira ambayo anatumia kusomea na kufundishiwa yawe mazuri na ndio maana wamewaandalia wanafunzi wanaoanza kidato mazingira mazuri ya kusomea na kuongeza kiwango cha ufaulu . 

Alibainisha kuwa ,madawati yote na viti 3,900 ambayo yanatengenezwa yana gharimu shilingi milioni 100 ambapo maamuzi ya kutengeneza madawati wenyewe yamewasaidia sana kwani wameweza kuokoa shilingi milioni 200 ambayo iwapo wasinge tengenezea katika karakana ya jiji wangetakiwa kuwalipa wakandarasi ambao wangetengeza . 

Akipokea madawati hayo Afisa elimu wa sekondari jiji la Arusha ,Valentine Makuka alimshukuru mkuu wa wilaya ya Arusha pamoja na mkurugenzi wa jiji la Arusha kwa kuwatengezea madawati kwani yatawaondolea adha ya wanafunzi ambao walikuwa wanakaa chini pamoja na wale ambao walikuwa wanabanana kwenye madawati . 

Alisema kuwa,madawati haya yatakithi mahitaji ambayo yalikuwa yamepungua kwa mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wanategemea kuwapokea Janury 6 mwaka 2020 ,huku akibainisha kuwa walijenga vyumba vya madarasa 26 ambavyo ni vipya na wanaamini yatakuwa yamekamilika hadi January 3 mwakani ili wanafunzi waweze kukaa na kusoma vyema . 

Aliongeza kuwa ,kwa mwaka huu wamepokea jumla ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 10,888 ambapo kabla ya madarasa haya walikuwa na upungufu wa madawati 3,999 lakini kwa uwepo wa madawati haya hakutakuwa na wanafunzi ambao watakaa chini kwa kukosa madawati . 

Kwa upande wake mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Thobias Chakwada alisema kuwa ,uwepo wa madawati hayo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi na kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hao ikiwa ni pamoja na kutoa motisha kwa wazazi kupeleka watoto kwa wingi mashuleni
Share To:

msumbanews

Post A Comment: