Mratibu wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la MEDO,  Idd Hashim, akiongoza majadiliano katika kongamano la kujadili changamoto dhidi ya wanafunzi wenye ulemavu wa akili katika Shule ya Msingi Mchanganyiko ya  Ilongero Halmashauri ya Wilaya ya Singida jana.
 Baadhi ya majengo yenye ubora yaliyo jengwa katika shule hiyo.
 Mratibu wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la MEDO,  Idd Hashim, akikagua miundombinu ya shule hiyo akiwa na viongozi wa kamati ya shule na wadau wa elimu wa Kata ya Ilongero.
 Mwalimu wa Kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili katika Shule ya Msingi Mchanganyiko ya  Ilongero, akizungumzia jinsi wanavyo wahudumia wanafunzi hao.
 Mwalimu Mkuu wa shule hiyo akizungumza.
 Mjadala ukiendelea.

Wanafunzi wakiimba shairi.
 Mwenyekiti wa shule hiyo, Rehema Mbura akizungumza.
 Choo cha kisasa kilicho jengwa shuleni hapo. 
 Diwani wa Kata ya Ilongero, Issa Mwiru, akijibu maswali ya wadau.
 Muonekano wa choo kilicho chakaa shuleni hapo.
 Ukaguzi wa choo kipya ukifanyika.
 Wanafunzi wakiwa darasani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kijiji cha Ilongero, Ibrahimu Mohammed akizungumza.
Na Waandishi wetu Singida. 
SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la MEDO limeendesha majadiliano na wadau wa elimu katika Shule ya Msingi Mchanganyiko ya Ilongero Halmashauri ya wilaya ya Singida kwa lengo la kuondoa changamoto zinazowakabili walemavu wa akili.
Akizungumza kwenye majadiliano hayo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani ambayo hufanyika Disemba 3 kila mwaka, Mratibu wa shirika hilo Idd Hashim alisema lengo la kukutana na wadau hao ni kuhakikisha watoto wenye ulemavu wa akili kutokubaguliwa katika Jamii. 
Alisema jamii ni lazima itambue walemavu ni watu kama watu wengine na kwamba ulemavu walionao hawakuhitaji bali unaweza kumpata mtu yeyote, hivyo jamii iache kuwaficha watu hao badala yake wawapatie haki zote za msingi ikiwemo elimu. 
"Wadau tuendelee kuelimisha jamii juu ya watoto wetu hawa tusiwafiche, na tuendelee kuiomba serikali iboreshe miundombinu ya shule."alisema Hashim. 
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Sijaona Nkurukwa alisema shule hiyo imeanzishwa mwaka 1951 huku elimu ya kitengo maalumu ikianzishwa mwaka 2015 ambapo watoto wenye ulemavu wa akili ni 29 wavulana wakiwa 18 wasichana 11.
Diwani wa kata ya Ilongero Mh:Issa Mwiru aliwasisitiza wananchi kulipa kodi ili serikali iendelee kuboresha miundombinu ya shule hasa kwa upande wa watoto wenye ulemavu wa akili, na kuwaomba viongozi na jamii kwa ujumla kuwajibika ili kuwaibua wazazi wanaowaficha watoto wao wenye ulemavu huko majumbani. 
Alisema kutokana na shule hiyo kupokea watoto katika maeneo mengi ya Halmashauri hiyo, hivyo jamii nzima kushirikiana kwa pamoja ili kuwaboreshea miundombinu ya kujifunzia watoto hao.
Aidha wazazi na wadau kwa ujumla walisema kuna baadhi ya wazazi wenye watoto wenye ulemavu huo wanashindwa kuwapeleka watoto wao shuleni kutokana na shule kutokuwa na mabweni ambapo inamlazima mzazi kumpeleka na kumrudisha nyumbani mtoto jambo ambalo ni gumu kwao hivyo serikali ingewajengea watoto hao mabweni. 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: