Wednesday, 18 December 2019

RC WA RUVUMA AIPONGEZA HALMASHAURI YA SONGEA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma  Christina Mndeme akikagua ukarabati wa majengo na madarasa katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songea mkoani humo wakati alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea

Na Amon Mtega ,Ruvuma
    MKUU wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani humo kwa kutekeleza miradi kwa wakati huku ikiwa imezingatia viwango vinavyohitajika.

 Pongezi hizo amezotoa  wakati alipokuwa akifanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali inyotekelezwa katika Manispaa hiyo ikiwemo ukarabati wa shule kongwe za Sekondari zilizopo mkoani humo.

 Mndeme wakati akifanya majumuisho ya ziara yake ambayo ilikuwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi [CCM] Wilaya ya Songea mjini amesema kuwa miradi aliyoiona imekuwa na viwango vinavyostahili na kuwa imetekelezwa kwa wakati.

”Nimepita kuangalia miradi mbalimbali mnayoitekeleza nimefurahishwa kuona fedha inayotolewa na Rais Dk,John Pombe Magufuli inatumika ipasavyo kwa manifaa ya wananchi “amesema mkuu huyo wa mkoa Christina Mndeme.

 Aidha akiwa katika kuangalia ukarabati wa majengo na madarasa kwenye shule kongwe za sekondari ambazo ni Sekondari ya wavulana ya Songea na Sekondari ya wasichana Songea aliwataka watunze miundombinu iliyowekwa ili kuendelea kuziweka shule hizo katika ubora wake.

 Hatahivyo katika shule ya Sekondari ya wasichana amewataka bweni moja ambalo ni kubwa liitwe jina la Magufuli ili kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Rais huyo.

  Pia mkuu huyo amechangia saruji mifuko 150 ambapo mifuko 50 katika shule ya Sekondari ya mazoezi Matogoro kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili na mifuko 50 katika Sekondari ya Londoni na mifuko 50 katika ujenzi wa Zahanati ya Likuyufusi kata ya Lilambo.

 Kwa upande wake mkurugenzi wa manispaa hiyo Tina Sekambo akizipokea pongezi hizo amesema kuwa ataendelea kuzingatia kanuni na maelekezo yanayotakiwa yafanyike katika utekelezaji wa miradi hiyo ikiwemo na agizo la ifikapo Januari mosi 2020 kituo kipya cha mabasi kilichopo kata ya  Tanga kitaanza kutumika ambacho kimetumia zaidi ya Sh.Bilioni sita[6)

 .

No comments:

Post a comment