Sunday, 1 December 2019

MA DC NA WATENDAJI RUVUMA WATAKIWA KWENDA KWA WANANCHI -RC MNDEME

  
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katikati akizindua huduma za bima ya Afya kwa jamii ,uliyoboreshwa kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro
...................................................................


     
MKUU wa mkoa wa Ruvuma ,Christina Mndeme amewataka wakuu wa wilaya pamoja ma watendaji wa mkoa huo kwenda kuhamasisha wananchi wajiunge kwenye mfuko wa bima ya Afya ya jamii (CHF)uliyoboreshwa ili kuwasaidia wananchi hao huduma za matibabu ,mwandishi    Amon Mtega anaripoti kutoka Ruvuma

   Wito huo ameutoa wakati akizindua huduma ya bima ya Afya iliyoboreshwa ndani ya mkoa huo ambapo wakuu wa idara mbalimbali pamoja na baadhi ya viongozi wa dini walihudhulia.

   Mndeme akizungumza kwenye uzinduzi huo alisema kuwa kila mwenye dhamana kwa wananchi wakiwemo wakuu wa Wilaya pamoja na watendaji wao wanawajibu wa kupita kuhamasisha wananchi wajiunge na mfuko huo.

 Amefafanua kuwa bima hiyo imeboreshwa ambapo kila kaya yenye watu wasiyozidi sita (6)wanauwezo wakujiunga kwenye mfuko huo kwa Sh.30,000/=kwa mwaka,na bima hiyo itatumika toka ngazi ya Zahanati hadi Hospital ya rufaa ya mkoa.

 Amesema kuwa Serikali imebuni mfumo huo ili kuboresha Afya kwa wananchi hadi kwa hali ya chini ambao siku za nyuma baadhi yao walikuwa wanashindwa kwenda kupata matibabu kutokana na vipato vyao kuwa vya chini jambo ambalo lilikuwa likiwaletea shida.

   "Nawaagiza wakuu wangu wa Wilaya pamoja na watendaji wenu kwenda kulisimamia hili kikamilifu ili wananchi waanze kupata huduma za matibabu" amesema Mkuu hiyo wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme.
   .

No comments:

Post a comment