Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali imeanza Warsha ya Usambazaji na Ukusanyaji wa maoni ya ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali [CAG]toleo Maalum kwa Mwaka wa Fedha ,ulioishia Tarehe ,30,2018.
Akizungumza katika ufunguzi wa Warsha hiyo jijini Dodoma ,Disemba 16,2019  kaimu mkurugenzi mkuu Ofisi ya Hesabu za Serikali,Benjamin Mashauri amesema kila mwananchi ana haki ya kupata taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote  huku akibainisha kuwa kupitia warsha hiyo wadau watapata fursa ya kuuliza Maswali na kujibiwa  pamoja na kukusanya maoni mbalimbali  na kuyafanyia kazi kwa manufaa ya ofisi ya CAG.
Aidha,Bw.Mashauri amesema lengo ni kuhakikisha kila mwananchi  anapata taarifa za kikaguzi zinazotoka ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ambapo  Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi watatoa Mada mbalimbali ambazo zinalenga kuelimisha wadau wote  ili kuweza kupata taarifa sahihi za ukaguzi.
Hata hivyo,Bw.Mashauri amezungumzia mafanikio  mbalimbali ya warsha  kwa miaka iliyopita ikiwa ni pamoja na  kuweza kufanya kazi kwa pamoja na asasi za kiraia , na vyombo vya habari kwa ukaribu zaidi,kuboresha kazi za kikaguzi.
Pia amezungumzia changamoto ya upatikanaji wa wana warsha walioshiriki katiaka warsha ya awali  na asasi kila mara kuteua washiriki wapya hali ambayo inaweza kusababisha kukosa mwendelezo wa masuala yaliyojadiliwa katika miaka iliyopita.
Kwa upande wake Afisa Habari wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali  Bi.Evelyne Thomas amesema  kila Mwaka huwa wanakuwa na Warsha kama hiyo ambapo Ofisi Ya Taifa ya Ukaguzi huwa inaandaa kijitabu kidogo  [CITIZEN]Ripoti ya Mwananchi,ambapo mwananchi mmoja mmoja huwa anapata fursa ya kukisoma na kukielewa pamoja na Mpango wa Kutoa elimu kwa wanahabari namna ya kuandika taarifa  kwa usahihi za Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: