>           Wananchi wakifyeka miti ovyo

Na Esther Macha,Mbeya

IMEELEZWA kuwa Wananchi wa Mikoa ya Nyanda za juu kusini wanaongoza kwa ukataji wa misitu kutokana na matumizi makubwa ya mkaa tofauti na nishati zingine ikiwemo gesi ya kupikia.

Hayo yamebainishwa na Meneja mahusiano wa Mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo alipokuwa akifungua Semina kwa wafanyabiashara ya usambazaji wa Gesi ya kupikia (LPG) kutoka Mikoa ya Nyanda za juu kusini akimwakilisha Mkurugenzi mkuu iliyofanyika jana jijini Mbeya.


Kaguo alisema kutokana na matumizi makubwa ya Mkaa Wananchi yam IKOA hiyo wanaongoza kwa kukata miti ovyo hivyo kuhatarisha mazingira ambapo ametoa wito kuanza kutumia gesi kwa kupikia.



Alisema matumizi ya gesi ya kupikia kwa mikoa ya Nyanda za juu kusini ni asilimia 8 pekee tofauti na Kanda zingine jambo linaloashiria  kuwa kuna ukataji wa miti sana pamoja na kutumia gharama kubwa kuupata tofauti na gesi.



Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa huduma kwa Wateja wa EWURA Kanda ya nyanda za juu kusini, Muhiba Chakupewa alisema Wananchi wanapaswa kuelimishwa juu ya umuhimu na urahisi wa matumizi ya gesi tofauti na Mkaa.



Alisema kwa kawaida mwananchi mmoja hutumia kilo 6 za mkaa kwa siku moja sawa na shilingi 24 ili hali anaweza kutumia kilo moja ya gesi ya kupikia kwa siku moja kwa gharama ya shilingi 1600

Alisema mbali na gharama ya gesi ya kupikia kuwa ndogo pia hurahisisha muda wa kupika pamoja na kutochafua vyombo kwa kuweka masizi tofauti na matumizi ya kuni na Mkaa.

Awali akizungumzia lengo la mafunzo kwa Mawakala ya Gesi za Kupikia, Meneja wa EWURA Kanda ya nyanda za juu kusini, Karim Ally  alisema ni kutokana na mkakati wa Mamlaka hiyo kuhakikisha gesi ya kupikia udhibiti wake unafanyika upya.

Alisema sekta ya Gesi ya kupikia haijadhibitiwa inavyotakiwa hivyo kupitia mafunzo wanayopewa Mawakala watasaidia kusambaza kwa wateja wao ambapo pia watapatiwa elimu kuhusu mfumo mzuri wa uuzaji na usambazaji.

Aliongeza kuwa katika udhibiti huo, Mamlaka inakusudia kutoa leseni kwa mawakala wa gesi ya kupikia ili waweze kufuata taratibu za uuzaji ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila muuzaji anakuwa na mzani wa kupimia gesi ili kutomwibia mnunuaji.

Aliongeza kuwa baada ya leseni hizo muuzaji ambaye hatakuwa na mzani wa kupimia gesi ya kupikia atapewa adhabu ambayo ni pamoja na faini isiyopungua shilingi Milioni tano (5,000,000).

Alisema katika masharti mengine ni kuhakikisha utunzaji wa mitungi ya gesi inazingatia usalama, kutofautisha rangi za mitungi kutokana na kampuni ya uzalishaji ili kumtofautishia mteja pamoja na kudhibii wizi.


Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: