Umoja wa wamiliki maduka ya Dawa baridi muhimu mkoani Pwani wafanya mkutano mkubwa wilayani mkuranga Kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali pamoja na Asasi za kiraia wilayani humo,

Akizungumza Kwa nyakati tofauti Mwenye kiti wa Umoja huo ndugu KITIKA aliiomba wizara ya Afya kupitia wilaya hiyo kujaribu kuondoa Baadhi ya Changamoto zinazowakuta wamiliki wote wa maduka ya dawa baridi wilayani humo kwani wanamsaada mkubwa Sana wa kuokoa maisha ya Watanzania Kwa ujumla,

Akizungumzia kuhusu Changamoto hizo ndugu KITIKA alijaribu kuzitaja ikiwapo na kucheleweshewa Kwa usajiri wa maduka hayo,Rushwa kukithiri na kutishiwa kufungiwa maduka sambamba na ukosefu wa wataalamu wa mafunzo katika idara hiyo wilayani mkuranga,

Pia Baadhi ya wamiliki na wadau mbalimbali waliojitokeza katika mkutano huo wameoimba serikali kupitia wizara husika kutambua na kutoa ushirikiano kwa wamiliki wa maduka ya dawa baridi kote Nchini kwani huu umoja ambao umeanzishwa mkoani Pwani (PWAMAO) umeonyesha kuzaa matunda katika wilaya zote ambazo Viongozi husika wametembelea Kwa kutoa semina Kwa wamiliki na ni Jambo ambalo limepokelewa vizuri Sana,

Naye Diwani wa kata ya mkuranga mh Muhidi alisifu umoja huo Kwa kusema, mchakato huu utasaidia kukuza hata mapato ya halmashauri ya wilaya ya mkuranga na hii ndiyo mkuranga tuitakayo, niwaahidi tu kuwa Kwa Kasi hii tutapiga hatua,

Vile vile Afsa tarafa wa wilaya ya mkuranga aliwataka wamiliki wote wa maduka ya dawa baridi kuwafichua wale wote wanaowakwamisha   katika mchakato wa kusajiri maduka ili offisi ya mkuu wa wilaya iweze kushughulika nao, pia Afsa tarafa huyo alionyesha kuhuzunika na kile kilichoelezwa na wamiliki hao kuwa ofisi ya Afsa Afya wilaya ya mkuranga ndiyo anakwamisha jitihada za usajiri na kupelekea maduka mengi wilani humo kuwa bubu(pasipo usajiri).
Share To:

msumbanews

Post A Comment: