Monday, 30 December 2019

R.D.O WAUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI WATUMIA BILIONI 1.4 KUFIKISHA MAJI VIJIJINI MUFINDI NA KILOLO

Mkurugenzi wa R.D.O Fidelis Filipatali akionyesha mfano wa miradi ya maji inayotekelezwa na taasisi yake 
Mkurugenzi wa R.D.O Fidelis Filipatali akizungumza na wanahabari juu ya kazi zinazofanywa na R.D.O 
Filipatali wa nne kulia akiwa na washiriki wa mdahalo wa amani na uzalendo baada ya kuwakilisha taarifa ya kazi za R.D.O 
Filipatali akipongezwa na Afisa wa polisi jamii mkoa wa Iringa Vicent  Msami


Katika kuunga mkono jitihada za  serikali ya awamu ya tano  chini ya Rais Dkt  John Magufuli kusogeza  huduma ya maji  safi na salama kwa wananchi vijijni  ,asasi isiyo ya kiserikali ya Rural Development Organization -(RDO) imetumia zaidi ya shilingi bioni 1.4 kupeleka  huduma ya maji safi na  salama kwenye kata  na vijiji zaidi ya 17 vya pembezoni mwa  wilaya ya Mufindi na Kilolo mkoani Iringa .

Mkurugenzi mtendaji  wa RDO ,Fidelis Filipatali  alisema  juzi  wakati mdahalo  wa kudumisha amani na uzalendo ulioandaliwa na mwamvuli  wa asasi  zisiyo ya kiserikali wa Iringa civil society organization( ICISO -Umbrella) kwa  ajili ya  kundi la wanawake ,vijana,asasi za  kiaria  pamoja na  viongozi wa  dini na vyama  vya siasa  mdahalo uliofanyika  mjini Mafinga katika   ukumbi wa shule ya Southern Highlands Mafinga .

"  Sisi kama  RDO  tunaisaidia  serikali katika mambo mbali mbali  yakiwemo ya kudumisha amani katika maeneo  yetu tunayofanyia kazi  kuona  wananchi  wake  wanafanya kazi kwa  amani na utulivu ila pamoja na kudumisha amani  tumekuwa  tukiungana na  serikali katika  kupeleka  huduma  ya  maji kwa wananchi  ambao  walikuwa hawana huduma  hiyo katika  wilaya ya Mufindi na Kilolo hasa  vijijini  "  alisema Filipatali 

Tumekuwa  tukijikita  zaidi  kuwawezesha   vijana  kupata  elimu ya  uzalendo na amani kwa  kuwawekea  misingi mizuri ya  kuja kujiajiri   wenyewe  kama  kuwapa elimu ya  ufundi  kwa  wale  ambao  walikuwa na ndoto za kukimbilia mijini pamoja  na  kuwapa nafasi ya  kufanya kazi katika miradi  ya maji .

Kuwa  hadi sasa  vijana  wengi wame wameweza  kuonyesha  uzalendo wao kwa kubaki vijijini  na kushirikiana na   wananchi kushiriki katika ujenzi wa miradi ya maji vijijini ambapo hadi sasa   vijiji takribani 17   na  vituo  vya kuchotea maji 230  vimepata  kujengwa katika  wilaya  za Mufindi na Kilolo .

Wakati  jumla ya  watumia maji 8500  wamekwisha  nufaika na  mradi  huo  wa maji  wa RDO  katika  wilaya ya Kilolo na Mufindi  ambao wanufaika hao ni wale ambao  walikuwa  awali  wakitumia maji ya mito yasiyo safi na salama  ila sasa  wanapata maji  ya  bomba  ambayo ni  safi na salama kama ilivyo kwa  wananchi wa  mijini.

" Kwa  kufanikisha huduma   hii ya maji  kufika  vijijini  wananchi  watakuwa na imani kubwa  na serikali lakini  pia  wataweza  kupata ajira  zaidi kwani  wanaweza  kutumia muda  wao kufanya shughuli za  kimaendeleo  badala ya  kupoteza  muda  kwenda  kutafuta maji  tambua huduma  zote  muhimu  kama maji  zikipatikana   vijijini  vijana  wanapenda  vijiji  vyao na Taifa na   kuacha kukimbilia  mijini na  huo ni mwanzo wa uzalendo  ndio maana  falsafa ya RDO sisi ni  vijijini  zaidi "

Alisema  kuwa  miradi  yao imekuwa  ikipewa nguvu  zaidi na kikundi  kidogo  cha  wakulima  kutoka Ulaya  ambao  wameweza  kujibana  wao na  familia  zao  ili  kusaidia  watanzania wa wilaya ya Kilolo na Mufindi  kuweza kupata  huduma ya maji  safi na salama pamoja na  kuwawezesha   vijana  kupata  elimu ya ufundi  kupitia  chuo cha ufundi  stadi  cha RDO Mdabulo na RDO Kilolo .

Hata   hivyo alisema kuwa taasisi  hiyo  imeamua  kuunga mkono jitihada zinazofanywa na  serikali kwa  kuwahudumia wananchi  katika  kuboresha  sekta ya  maji na elimu ya  ufundi   kwa  kuendelea   kusongeza  huduma ya maji kwa wananchi wa  pembezoni  ambao hawakuwa  na huduma   hiyo .

Kuwa RDO  wamefanikiwa  kwa  kiasi kikubwa  kushirikiana na  Halmashauri ya  wilaya  ya Mufindi  katika  uendelezaji  wa  upanuzi  wa miradi  ya maji safi  na salama  katika  kijiji  cha Nandala  na vijiji vingine  vya  wilaya ya Mufindi  kama Mpanga Tazara  ambako  ni  pembezoni kabisa mwa  mwilaya ya Mufindi  pamoja na vijiji vya  wilaya ya  Kilolo .

Filipatali alisema  shughuli  za usimamizi wa  miradi hiyo  zimekuwa  zikifanywa kwa ushirikiano  mkubwa  wa  serikali  za  vijiji  husika  na  miradi  hiyo  husimamiwa  na  wananchi  wenyewe  kupitia  jumuiya  za  watumiaji maji japo  changamoto zinazokabili  miradi  hiyo  kuwa ni kutowajibika  ipasavyo  kwa baadhi ya  watumiaji maji  kutotimiza wajibu wao pamoja na  baadhi ya  wanasiasa   kutumia  miradi hiyo  kujitafutia  umaarufu  wa  kisiasa .
Alisema  RDO  imejipanga kuendeleza upanuzi wa miradi ya maji katika  vijiji  ambavyo vina changamoto ya maji   baadhi ya  vitongoji  ambavyo  vilikuwa havina huduma  ya  maji kwenye  wilaya ya  Mufindi na  Kilolo lengo  likiwa ni  kuweza  kuwafikia  wananchi wenye uhitaji  wa  huduma   hiyo  .

No comments:

Post a comment