Meya wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza katika mahafari ya kituo cha Fahari Day Care  Wilayani Ilala Leo (Kulia)Mkurugenzi wa Kituo hicho Neema Mchau 
Meya wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto akiwa katika mahafari ya Kituo cha Fahari Day Care akizindua harambee ya ujenzi wa shule ya msingi 
Meya wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto akikabidhi vyeti Katika Mahafari ya kituo cha Fahari Day Care Wilayani Ilala Leo (kulia) Mkurugenzi wa Fahari Neema Mchau

NA HERI SHAABAN

Mstah wa Halmashauri ya Ilala Omary Kumbilamoto amezindua harambee kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Msingi  mradi wa Kituo cha Fahari Day Care .

Harambee hiyo iliendeshwa na Meya Kumbilamoto ambaye alikuwa mgeni rsmi katika mahafari ya kituo hicho kilichopo Wilayani Ilala.

Katika harambee hiyo aliwaeleza wazazi  akieleza siri ya mafanikio ya kushika nafasi ya tatu miaka mitatu  mfurulizo matokeo ya darasa la saba Halmashauri ya Ilala ambapo alisema  baadhi ya shule wanafunzi wanakula kila siku chakula.

 "Katika manispaa ya Ilala tunajivunia kiwango cha  ufaulu kupanda kila mwaka kutokana na kujenga mazingira bora ya shule na kuweka utaratibu wa kuwapa chai wanafunzi na mlo wa mchana kila siku " alisema Kumbilamoto.

Aidha alisema halmashauri ya Ilala ikiwemo Kata ya Vingunguti wanafunzi wamewekewa utaratibu wa kupata mlo kila siku
Wanafunzi  ambapo mwaka 2019 zaidi ya wanafunzi 23,000 wamechaguliwa darasa la saba .

Akielezea kituo hicho  cha Fahari Day Care  Kumbilamoto aliwapongeza kwa kuendeleza sekta ya Elimu katika Kata ya Gongolamboto wasitoze ada kubwa ili  waunge  mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya  Rais John Magufuli Mpango wa elimu bure .


Pia alisema Halmashauri ya Manispaa ya Ilala  itawasaidia Fahari Tuamke Maendeleo mchakato wa kutafuta eneo kwa ajili ya kujenga shule ya Msingi.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau ,alisema kituo cha fahari kilianzishwa mwaka 2014 na  kusajiliwa kwake 2016 dhumuni la kuanzishwa kwa kituo hicho kutoa elimu  bora yenye malezi mema kwa watoto kwa kuzingatia utamaduni wa Mtanzania.

" Matarajio yetu mwaka 2020 tuanzishe darasa la kwanza tuwe na shule kamili  inayomilikiwa na Fahari kwa sasa tupo katika mchakato wa kutafuta eneo La kujenga tupate eneo kubwa ndani ya wilaya ya Ilala " alisema Mchau.

Neema alisema katika Kata ya Gongolamboto wanashirikiana na Serikali katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kutoa misaada kusaidia shule za Serikali na kuandaa makongamano mbalimbali ikiwemo kuwaweka vijana Pamoja  na kuwawezesha kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali ili wajikwamue kiuchumi na kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda.


Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: