Mbunge wa Arusha Mashariki  akikata utepe kabla ya kutoa misaada kwa vikundi 
Mbunge wa Arumeru Mashariki John  Danielson Pallangyo ametoa msaada kwa Vikundi  vya wanawake wajane na watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwenye kitongoji cha Makisoru ,kijiji cha Nguruma kata ya Akeri Wilaya ya Arumeru .mwandishi wetu toka Arusha  Ferdinand Shayo anaripoti

Akizungumza wakati akikabidhi msaada wa shilingi milioni 1 kwa vikundi vya wanawake wajane wajasiraiamali ili kuongeza nguvu katika masuala ya kuweka akiba na kukopa kwenye vikundi vitatu vya Fanikiwa,Upendo na Wamebarikiwa  ambapo aliwataka kinamama hao kuendeleza vikundi na shughuli za uzalishaji mbali ili waweze kujikomboa kwenye dimbwi la umasikini.

Mbunge huyo pia alitoa ahadi ya matofali 1000 ya kusaidia ujenzi wa shule ya awali ya Elishadai ambayo inasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kutoka kaya zenye kipato cha chini ili waweze kupata elimu bora itakayowasaidia katika maisha.

John alisema kuwa serikali itaendelea kuunga mkono vikundi vya kinamama kwa kuwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi inayoelezea namna ambavyo vikundi hivyo vinaweza kuwa mkombozi wa kinamama na pia vinaweza kupata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri.

Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Arumeru Hungura Mbwana  ,aliwataka wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mbunge huyo katika kuwaletea maendeleo wananchi pamoja kuinga mkono serikali ya Dr.John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi nzuri ya kukarabati miundombinu ya barabara katika jimbo hilo.

Msimamizi wa Vikundi vya Wanawake wajasiriamali Bi.Regista Fredy alisema kuwa vikundi hivyo vimekua vikifanya shughuli mbalimbali ikiwemo ufagaji wa mbuzi wa maziwa ambao watagaiwa na Mbunge huyo wale ambao hawakupata ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mwanzilishi wa shule ya Elishadai Fred  Kulungwa alimshukuru Mbunge huyo kwa kuwapatia matofali 1000 ambayo yatasaidia kukamilisha ujenmzi wa shule hiyo ya awali ambayo ni hitaji kubwa katika kitongoji hicho.
Share To:

Francis Godwin Mzee wa matukiodaima

Post A Comment: