NA HERI SHAABAN
MBUNGE wa Segerea Bonah Ladislaus ameunda Kamati Maalum Wananchi wa Kata ya Kinyerezi Manispaa ya Ilala kwenda kuonana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Reli TRL kwa ajili ya fidia kupisha mradi wa Reli ya kisasa ambao umepita Mtaa wa Kifuru.
Kamati hiyo ilichaguliwa ya watu kumi Leo katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus ulifanyika eneo la Kifuru Wilayani Ilala kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi .
Akizungumza katika kikao hicho Bonah alisema dhumuni la mkutano huo kusikiliza kero za wananchi kuzifanyia kazi na kuelezea mafanikio ya miaka minne akiwa Mbunge wa Segerea yale aliotekeleza kwa wananchi.
Bonah alisema ziara hiyo ni endelevu anaongozana na Wataalam mbalimbali wakiwemo DAWASA kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya wananchi katika maeneo yenye changamoto ya Maji.
" Kata ya Kinyerezi umepita mradi wa Reli ya kisasa kuhusiana na suala la Fidia naomba tuchague Kamati maalum jumatatu tutaongozana kumuona mkurugenzi Mkuu wa Reli MHANDISI Kadogosa kujua malipo yenu mtalipwa lini ili kupisha mradi wa Serikali hivyo naomba msiwe na wasiwasi Serikali hii ni sikivu" alisema Bonah.
Bonah ameunda Kamati hiyo kufuatia wananchi zaidi ya 100 wapo njia panda wakisubili fidia kupisha mradi huo wa Reli ya Umeme.
Wakati huo huo ameunda Kamati ya kufatilia mradi wa Maji katika mtaa wa Kifuru ambapo Maji hayo yanatarajia kufika February mwaka 2020 .
Akielezea mafanikio yake kwa Kata ya Kinyerezi katika kuisaidia Serikali ya Rais John Magufuli sekta ya elimu ametoa fedha za jimbo la Segerea shilingi million 50 zimejenga madarasa sita pia fedha nyingine zimeweka umeme Shule ya MSINGI Zimbili na sasa wanafunzi wanasoma mazingira ya shule hizo yapo vizuri .
Pia aliezea mafanikio mengine alisema jimbo la Segerea kwa sasa Maji yapo kwa asilimia 90 maeneo yaliokosa Maji yatafika kwa wakati awali wakati anaingia madarakani mwaka 2015 maeneo mengi Maji yalikuwa hayajafika kwa sasa Maji yamefika kwa asilimia 90 .
Aliwataka Wanawake na Vijana waunde vikundi mbali mbali kwa ajili ya Mikopo ya Serikali ambayo inatolewa na Halmashauri ya Ilala aina riba kila kikundi kiandae Katiba washirikiane na Mama Maendeleo wa Kata watapewa taratibu za usajili.
Akielezea kuhusu Barabara za Mtaa alisema ameshazungumza na Mhandisi wa Tarura kuanzia Jumatatu barabara za Mtaa zote zitakarabatiwa.
Kwa upande wake Mhandisi wa DAWASA Tabata Julias Kulwa alisema Kata ya Kinyerezi Mtaa wa Kifuru watapata maji ya DAWASA kutokeq Kimara kwa sasa Maji yapo njiani na katika mikakati ya mwisho Mali ghafi za mradi huo zimekamilika iifikapo February 2020 wananchi wote watapata Maji.
Naye Polisi Kata Kinyerezi Peter Lusinde aliwataka waunde Polisi Jamii ili washirikiane na Jeshi la Polisi ili Kinyerezi iwe Salama katika kukomesha wahalifu.
Mwisho.
Post A Comment: