Tuesday, 10 December 2019

Kitunda Veteran washerekea Miaka 58 ya Uhuru kwa Bonanza


NA HERI SHAABAN
TIMU ya mpira miguu  Kitunda Veteran wamesherekea Miaka 58 ya Uhuru   kwa kufanya bonanza la mpira miguu na kushiriki katika kazi za kijamii.

Bonanza hilo lilifanyika Leo katika viwanja vya shule ya Msingi Kitunda ambapo kabla kuanza Bonanza  hilo walifanya usafi katika zahanati ya Kata   Kitunda na kutoa msaada  mbalimbali ikiwemo sabuni ,bomba za sindano na vifaa vya kujifungulia Wanawake.

MWENYEKITI wa Kitunda Veteran Ernest Komba alisema wanasherekea Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo sambamba na Miaka 13 ya Umoja wetu wa Kitunda Veteran tangu uanzishwe.

Komba alisema siku ya Leo ni muhimu katika Umoja huo wamepata mafanikio makubwa  tangu uanzishwe wameweza pia kuunda timu za vijana kwa ajili ya kutafuta vipaji vya michezo.

Aidha alisema  Kitunda Veteran wanaunga mkono Juhudi za Rais John Magufuli wameguswa na Utendaji kazi wake ikiwemo kupenda Sanaa ya michezo.

" Tunaitumia siku ya Leo katika bonanza hili wakikutana  timu ya Kiyombo Veteran  zote kutoka Kata ya Kitunda  katika sherehe za Miaka 13 tangu uanzishwe Umoja wetu " alisema Komba

Kwa upande Kaimu Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kitunda  Suzana Mpeku amewapongeza Timu ya Veteran Kitunda kwa kuwapa sabuni ,sindano ,na Vifaa vya kujifungulia katika hodi ya Wanawake.

Naye OFISA MTENDAJI wa Kata ya Kitunda alisema michezo ni AFYA,michezo ajira, michezo furaha pia kujenga udugu.

Beatrice aliwataka wadau wengine wa michezo kusaidia sekta ya afya .

Mwisho

No comments:

Post a comment