Saturday, 7 December 2019

KAMATI YA ULINZI MKOA WA RUKWA YAWEKA MKAKATI KUWABANA WANAOWAPA MIMBA WANAFUNZI


Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa  Rukwa imeweka mikakati mbalimbali kukabiliana na matukio ya uhalifu na wahalifu wakiwemo wanaowapa mimba wanafunzi  .mwandishi Elizabeth Ntambala anaripoti kutoka Rukwa 
 

 Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa ,mkuu wa mkoa wa Rukwa Joackim Wangabo na vyombo vya ulinzi ameazisha kampeni ya kuwasaka  wahalifu wote ambao wamekuwa wakijihusisha vitendo vya uhalifu pamoja na kuwapa mimba wanafunzi .


Mkoa umechukua hatua hiyo ikiwa  ni uungaji mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli  kuhakikisha kuwa kila mmoja anapata elimu bure bila malipo na hakuna vikwazo vyovyote .

Hivyo suala la ulinzi kwa watoto hao ni lazima na asiwepo wa kuwakatisha ndoto zao .


Katika kupambana na ulinzi wa wanafunzi  dhidi ya mimba  kwa kupitia mpango mkakati huo wa kutokomeza wahalifu wa mimba kwa wanafunzi
jeshi la polisi linachunguza makosa 27 ya tuhuma za mimba katika .

Kamanda Justine Masejo alisema kuwa kati ya hao wanafunzi waliopewa mimba kwa shule ya sekondari ni wanafunzi 20 ambapo kwa shule ya msingi ni wanafunzi 07 ambao ni wenye umri wa miaka( 15) hadi( 19)


Kamanda Masejo amewaomba wazazi kuwa karibu na watoto wao na wawafanye kuwa marafiki ili wasishindwe kuwashirikisha kwa lolote litakalo kuwa linawapata huko shuleni au katika mazingira yao ya kucheza kwani itapunguza au kuzuia kabisa mimba za utotoni.

Pia ametoa onyo kali kwa watu wote wanao jihusisha na vitendo vya ubakaji na hatufurahishwi navyo hivyo amewataka wananchi, wazazi kuwa mabalozi wazuri kutokana dhidi ya ulinzi wa mtoto kwani na kuacha kufumbia macho uhalifu .

No comments:

Post a comment