Monday, 23 December 2019

JESHI LA POLISI RUVUMA LATAKA WAZAZI KULINDA WATOTO SIKUKUU


Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Simon Maigwa akizungumza na vyombo vya habari mkoani humo kuhusina na Jeshi hilo lilivyojipanga kukabiliana na uharifu katika kipindi hiki cha Sikuku na vipindi  vingine.
.......................................................
Na Amon Mtega Ruvuma
    KAMANDA wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Simon Maigwa amewataka Wazazi na Walezi  wa mkoa huo kuongeza ulinzi wa kuwalinda Watoto wao katika kipindi hiki cha sikuku za Krisimas na Mwaka mpya ili watoto hao wasipatiwe madhara.

 Wito huo ametoa wakati akizungumza ofisini kwake  na Vyombo vya Habari vya mkoani humo ambapo  alielezea jinsi jeshi la polisi lilivyojipanga kukabiliana na uharifu ikiwemo kwenye sikuku hizo.

 Kamanda Maigwa amesema kuwa katika kipindi hiki cha sikuku kumekuwepo kwa baadhi ya Wazazi na Walezi kushindwa kuwa makini katika kuwalinda watoto wao jambo ambalo huwapelekea watoto hao kupatiwa madhara.

 Maigwa licha ya kuwataka Wazazi na Walezi kulinda familia zao lakini bado amewataka pia kuzilinda nyumba zao kuwa wasiziache bila mtu pindi wanapoenda kwenye nyumba za Ibada au kwenye matembezi ya kusherekea sikuku hizo.

 Katika hatua nyingine Kamanda huyo amewataka wale wote wanaofanya biashara za kumbi za starehe kuzingatia kanuni za kutowajaza watu kiasi cha kukosa hewa pamoja na kuacha kuweka   disco Toto ambazo zimekuwa zikiwahatarisha watoto.

 Aidha amewageukia wapangishaji wa nyumba za wageni wapangishe wageni hao kwa kufuata taratibu zilizowekwa ili kuwabaini waharifu wanaoenda kujificha kwenye nyumba hizo kwa visingizio kuwa wanasherekea sikuku.

 Hata hivyo amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kukabiliana na waharifu pamoja na kuimarisha ulinzi ikiwemo kwenye maeneo ya barabara kwaajili ya kuwathibiti madereva wazembe ambao wamekuwa wakisababisha ajali huku waengi wao ni waendesha Pikipiki(Bodaboda)wamekuwa wakibebana mtungo (Mishikaki)ambayo imekuwa ikipelekea kutokea kwa ajali .

                 

No comments:

Post a comment