Monday, 30 December 2019

Iciso na ushiriki Tanzania waanza kutoa elimu juu ya amani kuelekea uchaguzi mkuu 2020

Viongozi wa ICISO ,jeshi la polisi na MNGONET wakiwa katika picha ya pamoja na kundi la wanawake walioshiriki mdahalo wa amani ,uzalendo
Kundi la vijana katika picha ya pamoja 
Washiriki wakiwa katika mdahalo
Mwenyekiti wa MUNGONET Boniface Mlinga akitoa vitambulisho 
Mtendaji mkuu wa ICISO Raphae Mtitu akitoa elimu 


ASASI  isiyo ya  kiserikali ya Iringa society Organization (ICISO)  kwa  kushirikiana na  USHIRIKI TANZANIA chini ya  imeanza kuendesha  midahalo    kuwaandaa  watanzania  katika  ushiriki wa  uchaguzi  mkuu  mwaka 2020  kwa  amani  na uzalendo  pasipo kujiingiza  katika machafuko .

Akizungumza  wakati  wa  ufunguzi  wa mdahalo   ulioshirikisha  vijana  ,wanawake na  viongozi  wa taasisi  za  dini na vyama  vya  siasa  jana  katika  ukumbi wa Southern  Highlands mjini Mafinga  mtendaji  mkuu  wa  ICISO  Raphael Mtitu  alisema  kuwa   asasi  yake ni  miongoni mwa asasi  23  Tanzania  zinazowezeshwa  na USHIRIKI TANZANIA katika  kutoa  elimu  kwa  watanzania  juu ya elimu ya amani ,uzalendo  na ushirikishwaji .

Mtitu  alisema  kuwa  katika midahalo  hiyo  wamekuwa  wakizingatia mambo ya  msingi  kwa  ajili ya  kuwaandaa  watanzania   kushiriki  kwa amani na utulivu katika  uchaguzi  mkuu  na  kuwa  ushiriki Tanzania ni mtandao ambao unaunganisha  pamoja asasi 23 za  kiraia  zinazolenga   kujenga demokrasia  na utawala bora  kwa  vijana ,wanawake ,na  wenye  ulemavu  kwa  kuwajengea uwezo kupitia tafiti na mitandao ya  kijamii .

Aliema  kuwa  kupitia  midahalo  hiyo  ambayo  inafanyika katika wilaya  zote  za  mkoa wa Iringa kwa makundi  lengwa  zitasaidia   kukuza ushiriki  wa  wanawake ,vijana  na  wenye  ulemavu  kufanya mazungumzo  na kushirikiana na  serikali ya  Tanzania  katika  maamuzi  na utungaji  wa  ser hususani katika masuala ya  muungano .

Pia  kutetea sera  shirikishi  kwa  wanawake   ,vijana na  wenye  ulemavu  katika mchakato wa  uchaguzi   kutoa taarifa  kwa  umma  kuhusu  masuala  yanayohusu  wanawake  vijana na  wenye  ulemavu ,nafasi  ya  raia na mchakato wa  uchaguzi .

Mtitu  alisema kuwa  kupitia  midahalo  hiyo na  elimu wanayoitoa  wataweza  kuhamasisha  vijana  ,walemavu  na  wanawake  kujitokeza  kwa  wingi  katika  ushiriki  wa  uchaguzi  mkuu na  pamoja na kujitokeza  kugombea nafasi  mbali mbali .

Wakichangia  mada katika  mdahalo   huo  viongozi  wa taasisi  za dini  mchungaji  wa  kanisa la kiinjili la  kilutheri Tanzania  (KKKT  ) mtaa wa  Isalavanu   Bahati  Kitinusa   alisema  kuwa  wao kama  kanisa  wamekuwa  wakitoa  elimu  kwa  waumini  wao  namna gani ya  kuishi  kwa uzalendo na kudumisha amani  kupitia  ibada  zao .

Alisema  kuwa  mdahalo huo  umekuja  wakati sahihi  kwa  jamii ya  wilaya ya Mufindi  kujiandaa kudumisha amani  wakati wa  kuelekea  katika uchaguzi mkuu mwakani ambapo  kila mmoja analo  jukumu la  kuenzi  amani na uzalendo  wa Taifa  badala ya  kukubali  kutumiwa nawasio  penda amani  hii.

Huku  mchungaji  wa Kanisa la Triity  Ostari  Mafinga  Amani Kiwale  alisema  kuwa  dini ni nzuri  sana  na  viongozi  wa dini  ni wazuri  ila iwapo  watatumia  vibaya  midomo  yao na majukwaa ya  dini ni hatari  sana  kwa  ustawi wa Taifa   na  hivyo lazima  kwa viongozi wa  dini  kuwa mfano  mwema wakulinda ndimi  zao  wakati  wote .

Pia  alisema  kwa viongozi  wa siasa nao  wanajukumu la kudumisha amani  na utulivu wa nchi kwa  kutumia  vema  nafasi zao na kuepuka  kauli  zenye  vikwazo ambazo  zinaweza kuligawa  Taifa .

Huku   vijana   na wanawake  waliopata  kushiriki mdahalo huo  wakichangia mada katika mdahalo  mbali ya  kuponbeza asasi ya  ICISO kwa  kuwafikia  vijana  hao kupitia mdahalo  huo  bado  waliomba  elimu  hiyo  kuendelea  kutolewa  Zaidi  hasa   kwa  kuelekeza  vijijini  Zaidi ambapo  wengi hawajui  chochote .

Kwa  upande  wake  mkurugenzi  wa Rural  Development  Organization (RDO)  Fidelis  Filipatali  alisema  kuwa  suala la amani na uzalendo  limekuwa  likianza  kwa  kuwaandaa  vijana kuwa  wazalendo  kwa  kuwapatia elimu ya  ufundi  bure  pamoja pamoja na  elimu ya  kujiandaa  kimaisha .

Kwa  upande  wake  katibu  wa mtandao wa muungano wa  asasi  za  kiraia  wilaya ya Mufindi ( MUNGONET)  Renatus Mpiluka ambao pia  ni washiriki wa mdahalo  huo  wakijibu  swali la vijana  juu ya asasi  kwenda  vijijini  kutoa elimu kwa vijana na  walemavu  alisema  kuwa  asasi yake  na nyingine wamekuwa  wakitoa elimu  katika maeneo mbali mbali ya  wilaya   hiyo  alisema wao  pamoja na asasi za kiraia  wilaya  hiyo wamejipanga  kutoa  elimu  ya  uraia  kwa mpigakura  ili kujua  wajibu wao  kuanzia  wakati wa  kujiandikisha ,kampeni  ,kupiga  kura  na kuepuka  kushiriki  vitendo  vyovyote vya uvunjifu wa amani 

No comments:

Post a comment