Thursday, 5 December 2019

DC WILAYA YA SONGEA AWAPONGEZA WALIMU KWA KUONGEZA UFAULU


Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Pololet Mgema akiwapongeza walimu wa shule za msingi  wa Manispaa ya Songea ambao hawapo pichani kutokana na kupandisha ufaulu wa darasa la saba toka asilimia 79 hadi asilima 90.86. kulia ni asifaelimu wa shule za msingi manispaa ya Songea Zakia Fandey.
Walimu wakimsikiliza mkuu wa wilaya 

 Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Pololet Mgema amewapongeza walimu wa shule za msingi Manispaa ya Songea kwa kuongeza ufaulu wa darasa la saba toka asilimia 79 hadi kufikia asilimia 90.86.MWANDISHI AMON MTEGA ANARIPOTI TOKA RUVUMA

Akiwapongeza walimu hao wakati wa mkutano uliyowajumuisha walimu wa manispaa kwa lengo la kuwapongeza mkuu huyo alisema kuwa ufaulu umeongezeka ni kutokana na jitihada za walimu hao.

 Mgema amesema kuwa ni ukweli usiyopingika kuwa ufaulu umeongezeka ni kutokana na mpango mzuri wa walimu hao kufanya kazi kwa kujituma kwa kuhakikisha kila mwanafunzi anapata uelewa licha yakuwepo kwa baadhi ya changamoto mbalimbali.

 Aidha mkuu huyo aliwataka walimu hao kuendelea kuongeza bidii ya kufundisha ili mwakani waweze kufikia asilimia 95 au asilimia 100 huku baadhi ya changamoto zinazowakabili kama malimbikizo ya madeni mbalimbali yakiendelea kushughulikiwa .

“Natambua walimu mnafanya kazi ngumu sana na ni moja ya kazi ya wito ,ya kitume hivyo tunaomba muendelee kuwa na moyo huo huo ambao mwisho wa siku tutakuwa na taifa bora lenye wasomi wakubwa kupitia ninyi “alisema mkuu huyo wa wilaya ya Songea Pololet Mgema.

 Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inaendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kuimarisha miundombinu mbalimbali ikiwemo na utoaji elimu bure ambao umeleta matokeo chanya ya kuwepo kwa wazazi wengi kuwapeleka watoto wao shule.

  Kwa upande wake afisa elimu shule ya msingi manispaa ya Songea Zakia Fandey amesema kuwa waliamua kuweka mkutano huo na walimu wote wa manispaa hiyo ili kutambua mchango wao katika kazi ya elimu.

   Amefafanua kuwa hadi sasa wamejiwekea malengo ili ifikapo mwaka 2020 ufaulu uweze kuongezeka kuanzia asilimia 95 kwenda juu na siyo kurudi nyuma kwa kuwa tayari mpango wa KKK tatu umeimarika mashuleni.

  Mmoja wa walimu hao Siwetu Ahmad amesema kuwa mpango wa kuwaita walimu hao na kukaa nao pamoja kunawajengea imani ya kuendelea kuchapa kazi zaidi kutokana na mchango wao wa kazi  kutambuliwa.

“Hili jambo limetutia moyo walimu na sisi tuanaahidi kwenda kuchapa kazi kikamilifu kwa kuwa hata serikali imetambua mchango wetu tunasema asante kwa hilo”alisema mwalimu Siwetu Ahmad.

                        MWISHO.No comments:

Post a comment