Sunday, 3 November 2019

Yanga Kuvaana Tena Leo na Pyramids FC

Wawakilishi wa Tanzania, Yanga SC, Leo Jumapili wapo dimba la Ugenini nchini Misri kukipiga na Pyramids FC katika mechi ya marudiano kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho Barani Africa.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba, jijini Mwanza klabu ya Pyramids FC iliibuka na ushindi wa bao 2-1.

Mechi hiyo inatarajia kuanza saa tatu kamili ( 3:00) usiku.

No comments:

Post a comment