Na Lucas Myovela_Arusha.


Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Paramagamba Kabudi amezitaka nchi za jumuiya ya Afrika mashariki kuwekeza katika sekta ya miundo mbinu ili kuwa na nishati ya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa viwanda .

Amesema hatua hiyo itawezesha biashara kukua kwa nchi za jumuiya hiyo kiwemo kuongeza sayansi ,Teknolojia na ubunifu kwa Vijana wenye ujuzi wa kufanyakazi kwenye viwanda  hivyo.

Ameyasema hayo katika mkutano wa Wafanyabiashara zaidi ya 1000 wa nchi za Afrika mashariki ulioandaliwa na Baraza la Wafanyabiashara wa nchi za Afrika  Mashariki (EABC) unaofanyika kwa siku mbili jijini Arusha na kwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 20 ya jumuiya ya Afrika Mashariki.

Prof.Kabudi amesema kuwa,nchi zilizo nyuma katika maendeleo ya viwanda zinapaswa kusaidiwa ili kupata viwanda  na kuweza kuzalisha bidhaa na kuuza kwenye soko la pamoja la jumuiya ya Afrika Mashariki.

"lazima nchi ziwe na viwanda vya kutosha na kufanyabiashara nzuri ,kwa sababu jumuiya ni ya  watu wote na lazima iwanufaishe wananchi wote"Amesema


Naye waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amesema kuwa uchumi wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki lazima ujengwe kupitia sekta binafsi za viwanda,kilimo, Mifugo na kuimarisha miundo mbinu .

Amesema serikali ya Tanzania inajitahidi kuweka mazingira Bora kwa wafanyabiashara ili biashara zao zinakua na kuhakikisha wanafanyabiashara  nje ya Tanzania bila kikwazo chochote .

Waziri Bashingwa ametumia wasaa huo kuwakaribisha wawekezaji kuja hapa nchini kuwekeza viwanda kwa ajili ya vifungashio na kuviuza katika nchi wanachama.

Baadhi  ya Wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo,Jiten Shah Mwanzilishi wa kampuni ya QICK MARC,wanashukuru kwa mashirikiano mazuri kwa nchi za Africa,kuwarahisishia Wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa urahisi zaidi,na kupenda kuzidi kuendelea kuweka hapa nchini na Africa lwa ujumla wake.

"Mpaka sasa kampuni yetu inafanya kazi vizuri katika nchi za Africa,kwasasa tunafanya kazi na nchi ya kenya kiukweli wapo vizuri nasasa tunakuja nchini Tanzania kwaajili ya uwekezaji,mbali na changamoto za kibiasha Tanzajia bado inayo fursa nyingi za uwekezaji na sisi kama Quick Marc,tutazidi kuwekeza bidhaa zeth na biashara zetu katika nchi za Africa kikubwa viongozi waweke usawa sahihi wa kibiashara kwa nchi za Africa ya Mashariki".Alisema Jiten Shash. 


Naye  Erhard  Mlyansi ambaye ni Afisa masoko mkuu wa kampuni ya Motisun Group kutoka jijini Dar es Saalamu inayotengeneza bidhaa mbalimbali vya ujenzi na juisi ya Sayona na kuishikuru EABIS kwa kutuweka pamoja wafanyabiashara pamaoja na wawekezaji ili kuweza kupanua masoko na uwekezaji.

"Katika viwanda vya utengenezaji wa mabati hapa nchini sisi pekee ndiyo tunao tengeneza hidhaa zetu hapa hapa nchiji tofauti na makampuni mengine wao wanaagiza nje na wanakuja kukunjia migogo hapa nchini,Kwa mabati yetu ji bora zaidi kuliko mengine hata leo mtu akitumia bidhaa zetu au Mabati yetu ya KIBOKO yanadumu zaidi ya miaka mitano pasipo kupauka wala kupoteza muonekano wake".Alisema Erhard.










Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: