Friday, 29 November 2019

"VIAPO VYA WENYE VITI SERIKALI ZA MITAA NA VIJIJI VYA FANA MKURANGA

Jana tarehe 28/11/2019 lilifanyika tukio la kihistoria na la Aina yake katika Wilaya ya mkuranga mkoani Pwani, Baada ya Viongozi wa ngazi ya serikali za mitaa na vijiji katoka katika Kata ya MwandegeKula viapo wilayani hapo,

Alikuwa ni Hakimu wa wilaya hiyo ambapo aliwapisha Viapo vya utumishi viongozi hao ambao walishinda nafasi hizo katika mchakato wa uchaguzi uliomalizika hivi karibuni ngazi za mitaa na vijiji,

Wakati wa Kula viapo hiyo vya Uongozi, Viongozi hao kutoka katika Kata Mwandege wilaya ya Mkuranga waliahidi kuwatumikia wananchi wote bila kujali Dini, wala itikadi za vyama Bali watafanya kazi Kwa maslahi ya wananchi waliowapa dhamana katika maeneo Yao husika ,

Pia wajumbe wa halmashauri ya vijiji nao Kwa wakati wao waliahidi kuonyesha ushirikiano Kwa viongozi hao wa ngazi za mitaa na Vijiji na kuahidi kuchapa kazi kama walivyo ahidi kwenye kampeni zao.

Pia Viongozi mbali mbali waliohudhuria hapo waliwapa moyo viongozi wanaoingia madarakani kuwa wafanye kazi bila woga na kuwafikia wananchi popote pamoja na kutatua kero katika maeneo korofi katika mitaa na vijiji vyao.


#uzalendokwanzakwamaendeleoyataifa

No comments:

Post a comment