Na Heri shaaban
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM )Taifa imemuonya Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazarendo Zito Kabwe ache kutumika na Mabeberu wa kisiasa .

Tamko hilo limetolewa Dar es Salaam leo na Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Leonard Singo wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari kuwapongeza Vijana wa UVCCM   Kuchukua fomu ,kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kumpongeza Rais John Magufuli kwa uteuzi wa Mkaguzi Hesabu za Serikali CAG .

"Tunamuonya Zito Kabwe anachofanya UVCCM tunakijua pamoja na kundi lake aache kutumika na mabeberu wa kisiasa tunamuomba akae kimya"alisema Leonard .

Leonard alimtaka Zito kabwe akae kimya asipotoshe watanzania Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli    inafanya kazi zaidi ya mafuriko katika utekelezaji wa ilani na kuleta maendeleo.

Ameshangazwa wana siasa uchwara wanaendelea kumpinga Rais John Magufuli wakati wasomi na wachumi wanaunga mkono juhudi za Rais.

Aidha alielezea wimbi la kufa kwa vya vya siasa Tanzania akisema kunatokana na kasi ya utendaji kazi wa Rais wa awamu ya tano katika kujenga Tanzania ya  uchumi wa viwanda.

Leonard alisema Chama cha Mapinduzi CCM kinaongozwa na Katiba na sheria sio chama cha SACOS kama vingine hivyo alivionya vyama vya Siasa viache kuchonganisha badala yake washirikiane katika kuleta maendeleo ili kukuza uchumi wa nchi.
 
Akielezea Watumishi wa Serikali ambao wanapinga utendaji kazi wa Rais John Magufuli alisema kama wapo naomba wakae chonjo kabla  chama akijawatoa katika nyazifa zao

 Akizungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa aliwapongeza vijana wa  UVCCM  pamoja na chama kwa kuwamini pamoja na Katibu Mkuu Bashiru Ally kwa kupinga Rushwa na kuwapa dhamana vijana.

Wakati huohuo UVCCM Taifa  inakemea mambo ya ovyo katika mitandao ya kijamii na kuomba vyombo vya sheria kuwachukulia hatua mitandao ya kijamii yote ambayo inaichafua serikali iliwemo kupinga yale mazuri ambayo anawatekelezea wananchi katika kuleta maendeleo.

 "Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi na TCRA tunawaomba mfatilie na kuwachukulia hatua ili kundi la wachache ambalo linatumia mitandao ya kijamii kukosoa serikali kila wakati"alisema.
MWISHO

Pres UVCCM
Taifa Novemba 04/2019
Share To:

msumbanews

Post A Comment: