Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania TEMESA umefanikiwa kuboresha na kusimamia uendeshaji wa Vivuko vya Serikali nchini kwa kuendelea kuongeza idadi yake kutoka kumi na tatu wakati wakala ukianzishwa 2005 hadi kufikia thelathini pamoja na boti ndogo tano.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji mkuu wa TEMESA  nchini Mhandisi  Japhet Maselle wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ,ambapo amesema idadi hiyo ni ongezeko la vivuko kumi na saba.

“Wakala kwa sasa inatekeleza ujenzi wa vivuko vipya kwa ajili ya maeneo ya Mafia-Nyamisati  ambao unagharimu  Bilioni 5.3 ,Bugorola –Ukara  Bilioni 4.2,Chato-Nkome unagharimu Bilioni 3.1 na Kayenze –Bezi Tsh.Bilioni 2.7.Ujenzi wa Vivuko vyote hivi unagharimu fedha za
Kitanzania Tsh.Bilioni 15.3.”amesema.

Mhandisi Maselle amesema TEMESA kwa kushirikiana na Wizara wanaandaa mfumo wa TEHAMA ili kudhibiti uzito wa abiria na mizigo inayobeba na pia kuhakikisha usalama wa mali.

“TEMESA pia imejipanga ufungaji wa vifaa vya TEHAMA  ikiwa ni pamoja na CCTV Camera kwa ajili ya Usalama na kurahisisha ufanyaji kazi,mfano kuna kuandaa mfumo wa wa usimamizi na ufuatiliaji wa mienendo ya vivuko kwa kudhibiti uzito  wa abiria na Mizigo inayobebwa  kwenye
vivuko[Ferry Management System]”Amesema.

Aidha amegusia juu ya uboreshaji wa karakana za kutengeneza magari ya Serikali ambapo amesema kuwa hadi sasa wakala huo una karakana 26 katika Mikoa yote ya Tanzania na vifaa vyote vikiwemo vipuri vipo vya
kutosha kwa ajili ya kazi.

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania TEMESA ulianzishwa chini ya Sheria ya Wakala namba 30 ya mwaka 1997 ambapo ilikasimiwa karibu majukumu yote yaliyokuwa yanatekelezwa na Idara ya Ufundi na Umeme chini ya Wizara ya miundombinu, lengo likiwa kutoa huduma bora katika Nyanja za Uhandisi mitambo,umeme,Elektroniki na Uendeshaji Vivuko.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: