Saturday, 30 November 2019

MADIWANI MOROGORO WAJIFUNZA UKUSANYAJI MAPATO ILALA

Naibu meya wa halmashauri ya Ilala Ojambi Masaburi akizungumza na Madiwani wa Morogoro katika ziara ya manispaa ya Ilala kuangalia wanavyokusanya mapato (kulia )Meya wa Manispaa ya  Morogoro Pascal Kihango
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Sheila Edward akizungumza Manispaa ya Ilala leo na Wakuu wa Idara na Madiwani katika ziara ya kujifunza Ilala walivyofanikiwa kukusanya Mapato na Usafi
Mkuu wa Wilaya ya  Morogoro Regina Chojo akizungumza na Madiwani na Wakuu wa Idara wa Manispaa ya Ilala leo katika ziara ya kujifunza Ilala jinsi wanavyokusanya mapato na masaswala ya usafi,(kushoto )Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto

..................................................

Picha na habari na Heri Shaaban

MADIWANI wa Manispaa ya Morogoro wamefanya ziara ya mafunzo halmashauri ya Ilala kuangalia wanavyokusanya mapato  ili wakafanye katika manispaa yao.

Katika ziara hiyo madiwani waliongozana na mkuu wa Wilaya ya Morogoro ,Regina Chonjo,Mkurugenzi wa manispaa hiyo Sheila Edward  na Wakuu wa Idara  ambapo msafara huo ulipokelewa na Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto .

Akizungumza katika    mafunzo hayo mkurugenzi wa Manispaa  Morogoro Sheila Edward  alisema dhumuni la ziara yao Halmashauri ya Ilala kuangalia  jinsi walivyofanikiwa katika ukusanyaji mapato ili wakaige katika manispaa ya Morogoro.

"Morogoro inatakiwa kuwa Jiji ila kwanza kabla kuwa jiji lazima ifanye vizuri katika kukusanya mapato   ivuke malengo tujue Ilala mbinu walizotumia  kupata mapato makubwa"alisema Sheila.

Sheila aliwataka Watendaji wake pamoja na madiwani wa Morogoro kutumia mafunzo hayo na elimu waliyopata iwe chachu ya kuongeza mapato katika manispaa yao.

Aidha alisema mara baada mafunzo hayo   watakwenda kufanya kazi kwa weledi katika ukusanyaji mapato ili wafikie lengo la asilimia 100.

Pia alisema mbinu nyingine waliojifunza halmashauri ya Ilala  madiwani wake na wakuu wa idara katika  idara ya usafi  jinsi Ilala wanavyofanya usafi ambapo alisema elimu hiyo wataitumia katika manispaa yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Regina Chonjo alisema standi ya Kisasa ya mabasi ya Morogoro kwa sasa ipo chini ya halmashauri kwa siku inaingiza shilingi milioni 4.

Mkuu wa Wilaya Chonjo alisema lengo la ziara yao Ilala kuja kujifunza Manispaa ya Morogoro wanakusanya mapato ila vipo vitu vya kujifunza ili wakafanye vizuri zaidi.

Alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa awamu ya tano John Magufuli katika kukuza  Tanzania ya uchumi wa Viwanda na kasi ya miradi ya maendeleo na miradi Mkakati.

Aiwataka wananchi wake kujishughulisha na kufanya shughuli za uzalishaji mali bila kubughuziwa..

Naye Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto amewataka madiwani wa Manispaa ya morogoro kujenga mauhusiano yao kwa pamoja na kushirikiana katika kuisaidia serikali   kujenga Tanzania ya viwanda.


No comments:

Post a comment