Meneja wa Kampuni ya  Ujenzi ya Elemech Engineering, Suraj Kashkar (kushoto) akifanya majadiliano  na Katibu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) Mkoa wa Singida, Tupilike Njela, kuhusu hatma  ya stahiki za wafanyakazi waliochini ya kampuni hiyo.
 Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa kazini.
 Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa kazini.
 Wafanyakazi wa kampuni hiyo , wakimsikiliza Katibu Msaidizi wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) Mkoa wa Singida, Tupilike Njela.
 Mwanasheria wa kampuni hiyo,  Joseph Futakamba wakati akizungumza na wafanyakazi hao.
 Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakifurahia baada ya maazimio ya kikao hicho.
 Sehemu ya mradi unaojengwa na kampuni hiyo.
Sehemu ya mradi unaojengwa na kampuni hiyo.
Na Waandishi Wetu, Singida
 KAMPUNI  ya Ujenzi ya Elemech Engineering inayojenga kituo cha kupokea na kupoza umeme mkoani Singida kuwalipa mafao wafanyakazi wake baada ya mkataba wa kazi kumalizika.
Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Mwanasheria wa kampuni hiyo Joseph Futakamba wakati akizungumza na wafanyakazi hao waliotaka kujua hatima yao baada ya kampuni hiyo kumaliza mkataba wa kazi waliyopewa na kampuni mama ya KC.
"Wafanyakazi wote watapata stahiki zao zote baada ya mkataba wa kazi kumalizika kama sheria za kazi zinavyoelekeza" alisema Futakamba.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni hiyo Yusuph Bisech alisema kwa umoja wao walipenda kujua kuhusu stahiki zao baada ya mkataba huo wa kazi kumalizika.
Alisema wamefanyakazi kwa moyo wa kizalendo  na kujituma kwa muda wote wa kampuni hiyo ikiwa ndani ya mkataba huo hivyo matumaini yao ni kuona wanapata stahiki zao ili wakaanze maisha mapya huko majumbani kwao.
Mwakilishi kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Taasisi za Fedha na Huduma za Ushauri (TUICO) Mkoa wa Singida, Tupilike Njela alisema wafanyakazi hao wote watalipwa mafao na stahiki zao.
" Hawa wafanyakazi walikuja kutaka kujua hatima yao baada ya mkataba wa kazi wa kampuni hiyo kumalizika ndio maana tumefika hapa kuzungumza na uongozi wa kampuni hii ili kujua ilivyojipanga kuwalipa wafanyakazi hao" alisema Njela.
Alisema baada ya kikao cha mazungumzo kwa pande zote walifikia muafaka ambapo pia wafanyakazi hao watapewa cheti kitakacho watambulisha kufanyakazi katika makampuni kutokana na kazi nzuri waliyoifanya katika kampuni hiyo ya  Elemech Engineering.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: