Saturday, 30 November 2019

ELIMU YA UMEME KWA WASIOONA YAIPA TANESCO TASWIRA MPYA


 MKUU wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare  akizungumza wakati wa uzinduzi wa wasrha hiyo kushoto ni  Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro William Masome
 Sehemu ya wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro.
 Sehemu ya wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro Mkuu wa Mkoa huo ambaye hayupo pichani

 wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro.


MKUU wa Mkoa wa Morogoro aliyevaa suti jeusi akiwa kwenye picha ya Pamoja na washiriki wa semina hiyo kushoto ni  Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro William Masome 

SHIRIKA la Umeme Nchini TANESCO limeendesha semina maalum inayohusu masuala ya Umeme kwa wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati wa uzinduzi  wa warsha hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Loata Ole Sanare amesema kuwa Tanesco  imeonyesha mfano mzuri wa kuigwa kwa kutoa elimu hiyo kwa watu wa kundi  maalum katika jamii.

Alisema pia kupitia hili shirika limetoa taswira kuwa mashirika ya Umma yanafuata muelekeo wa Raisi John Pombe Magufuli ambae ni  Raisi wa wanyonge na kwa kujali wateja wake hata wa Makundi maalum kwa kutoa elimuYa Umeme itakayowasaidia katika maisha yao ya kila  siku.

Mkuu huyo wa Mkoa  amewataka wasioona kutokuwa wanyonge kwakudhani kuwa  Serikali haiwatambui na kusema kuwa Serikali ipo pamoja nao na kuwakaribisha katika ofisi za Mkoa, muda wowote watakapokua na changamoto zozote.

Naye Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro William Masome amesema Kuwa TANESCO chini ya Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Tito Mwinuka imetambua umuhimu wa watu wenye Ulemavu wa kutoona kupatiwa elimu ya Umeme ili waweze kutambua fursa  zitokanazo na umeme zitakazoweza kuwainua kiuchumi lakin pia kuwafundisha jinsi ya kutumia umeme vizuri (matumizi Bora ya umeme)ili wasilipe gharama kubwa
Kwenye kununua Umeme.

Naye kwa upande wake Mratibu wa idara ya maendeleo, Vijana na Chipkizi toka TLB , Bw.Kiongo Itambu ameishukuru TANESCO kwa kuwapatia elimu hiyo
Maalum ambayo itawasaidia hasa katika kujiepusha na matukio ambayo yanaweza kuathiri usalama wao.

Alisema kwani wameshajua athari za kukaa karibu na miundombinu ya umeme  na  kuahidi kushirikiana na TANESCO katika kuwafichua wanaolihujumu Shirika kwa kuiba umeme na kuharibu miundombinu ya Shirika.

Aidha Bw. Kiongo alimuhakikishia Mkuu wa mkoa kuwa wao kama watu wenye ulemavu ni kama watu wengine, ni mara chache kusikika wasioona ikiwa na sifa ya kuliibia shirika la umeme na watakuwa mabalozi wa kuhakikisha Tanesco haiujumiwi ili kukuza kipato chake kwa maendeleo ya Shirika na Taifa kwa ujumla

No comments:

Post a comment