Monday, 7 October 2019

TANZIA: Mtunzi wa wimbo 'Chadema People's Power' afariki dunia.


Aliye kuwa Mkuu wa Idara ya sanaa CHADEMA makao makuu Fullgency Mapunda ( Mwana Cotide) amefariki dunia saa 10 :20 usiku huu wa tarehe 06/10/ 2019 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Taarifa kamili ya wapi msiba utakuwepo itatolewa kesho na familia ya marehemu.

Alikuwa amelazwa katika Hospitali ya St Monica iliyopo Manzese Jijini Dar alikokuwa akipatiwa matibabu. Enzi za uhai wake aliimba wimbo wa chama hicho wenye maneno "CHADEMA People's Power" ambao ni maarufu.

No comments:

Post a Comment