Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda jana October 05 amewasilisha kwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM kuanzia ngazi ya Taifa, Mkoa,Wilaya, Kata na Mashina taarifa ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Tano kwenye Mkoa huo kwa mwaka 2019 ikiwa ni sehemu ya Utekekelezaji wa Ilani ya CCM inayolenga kutatua kero za Wananchi.

RC Makonda amesema miongoni mwa miradi inayotekelezwa kwenye mkoa huo ni Ujenzi wa Barabara chini ya TANROAD, TATURA na DMDP zenye urefu wa Km 5,153, Ujenzi wa Miundombinu ya upatikanaji wa Maji, Ujenzi wa Mejengo ya Hospital, Vituo vya Afya, Zahanati na Vifaa Tiba ambavyo vimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto kwa wananchi.

Aidha RC Makonda ameitaja miradi mingine inayotekelezwa ni sekta ya Elimu kupitia ujenzi wa Vyumba vya madarasa, ofisi za walimu na matundu ya Vyoo, Sekta ya Nishati ya Umeme, Ujenzi wa Viwanda, Sekta ya Ardhi, Usafiri pamoja na suala la Ulinzi na usalama.

Kwa Upande wake katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Dkt. Bashiru Ally amepongeza mkoa wa Dar es salaam kwa kazi kubwa na nzuri ya kuwaonyesha wananchi kwa vitendo kile kinachofanywa na Serikali yao ya Awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Aidha Dkt. Bashiru amepongeza Mkoa huo kwa kuwa kinara wa kusimamia makusanyo ya kodi, kusimamia kikamilifu suala la ulinzi na usalama, kusimamia Usafi wa Mazingira pamoja na kuwa na utamaduni mzuri wa kushirikiana na Wasanii na vyombo vya habari.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: