Saturday, 19 October 2019

HALMASHAURI YA ILALA WAZINDUA CHANJO YA SURUA NA LUBELA


NA HERI SHAABAN

HALMASHAURI ya Ilala imezindua chanjo ya magonjwa ya Surua na Lubela katika uzinduzi huo  wamewapa mafunzo Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Maofisa Watendaji Kata.


Akizungumza katika uzinduzi huo kwa Wenyeviti na Maafisa watendaji wa kata Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala Jumanne  Shauri , alisema Manispaa wametenga vituo 182 zahanati,vituo vya afya,hospitali na ofisi za serikali za Mitaa zote.

Shauri alisema  kampeni hiyo ya chanjo shirikishi surua na rubela katika manispaa ya Ilala imeanza Octoba 17 mpaka Octoba 21 chanjo ya surua na rubela  walengwa watoto kuanzia miezi 9 mpaka miaka mitano na polio kwa watoto wa mwaka mmoja na nusu hadi mitatu na nusu.

"Walengwa katika halmashauri ya Ilala surua na rubela matarajio kuwafikia watoto 191,502 polio ya sindano kuwafikia watoto 113,797"alisema shauri.


Shauri aliwataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kushirikiana na Serikali katika kampeni hiyo ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Aidha aliwapongeza Wenyeviti wa Serikali za Mitaa walio maliza muda wao  katika kuwatumikia wananchi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa halmashauri ya Ilala   Dkt,Emmily Lihawa alisema Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo imeanda  chanjo hiyo ya Kitaifa.

Dkt ,Lihawa alisema   dhumuni la kampeni hiyo kupambana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ambayo ni ugonjwa wa surua ,rubela na polio dhumuni kuongeza kinga kwa watoto wote kwa kuwapatia chanjo.

Alisema hata kama wamepata chanjo hizo katika utaratibu wa kawaida wa kutoa huduma za chanjo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya .

Alisema surua ni ugonjwa unaosababishwa na  virusi aina ya "morbillivirus paramyxovirus vinavyoenezwa kwa njia ya hewa .

Alitaja baadhi ya dalili za ugonjwa wa surua pamoja na homa,mafua,kikohozi,macho kuwa mekundu ,kutoa maji maji na vipele vidogo vidogo ambavyo huanza kwenye paji la uso nyuma ya masikio na kusambaa usoni na mwili mzima .
MWISHO
Octoba 19/2019

No comments:

Post a comment